Anayedaiwa King Bae wa Zari Avunja Ukimya

MIONGONI mwa watu wanaotafutwa (most searched) kwenye mitandao ya kijamii Kibongobongo ni pamoja na mtu anayetajwa kwa jina la King Bae ambaye mwanamama Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ amekuwa akitamba kufunga naye ndoa kisha kumficha sura yake kukwepa nyakunyaku wa waume za watu.

 

Baada ya kutengana na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zari ambaye ni mama wa watoto watano, anadaiwa kuwa kwenye uhusiano na jamaa huyo anayesemekana kuwa na ukwasi wa kutisha aliyedai kufunga naye ndoa mwezi Julai, mwaka huu.

 

Katika kipindi chote hicho, Zari amekuwa akisababisha kila mwanaume anayekuwa karibu naye kuhisiwa ndiye King Bae.

 

Galston Anthony; huyu ni mmoja wa wanaume wengi ambaye anahisiwa ndiye King Bae, jambo ambalo linampa wakati mgumu. Watu wengi, hasa kurasa za udaku za Instagram wanaamini Zari amekuwa akidanganya kuwa na mwanaume mpya baada ya kuachana Diamond au Mondi na kumuita Mrs Hewa.

Kwa upande wake, Anthony anayedaiwa kuwa ndiye King Bae amevunja ukimya na kuwataka watu kuacha kumchanganya na King Bae. Jamaa huyo anasema kuwa watu waache kumhisi kwani yeye ni meneja wa Zari tu na si vinginevyo na kwamba yeye ni mume wa mtu ambaye amemuoa mwanamke ajulikanaye kwa jina la Nandi na wana familia na watoto.

Anthony anasema muda wote amekuwa akimuonesha Zari upendo wa kikazi zaidi huku akimuita jina la ‘Dada Mkubwa’ na kumpa heshima yote anayostahili. Jamaa huyo ambaye ni raia wa Afrika Kusini ‘Sauz’, katika moja ya mahojiano yake nchini humo, anawaomba watu kuacha kumchanganya au kumhisi kuwa ndiye King Bae.

Zari na Mondi walidumu kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa takriban miaka minne na kujaliwa watoto wawili, Tiffah na Nillan kabla ya kutengana Februari 14, mwaka jana. Baada ya hapo kila mmoja alichukua hamsini zake ambapo Zari amekuwa akitamba kuolewa na huyo King Bae huko Mondi akitua kwa Tanasha Donna Oketch ambaye ni mtangazaji kutoka Kenya.

Toa comment