testiingg
The House of Favourite Newspapers

Anayedaiwa Kukausha Sehemu Za Siri Na Kuzisaga Afikishwa Mahakamani

0

 

 

Mganga wa Kienyeji (Katikati)  akiwa na washtakiwa wenzake wawili   wakiwa katika Mahakama ya akimu mkazi wilayani Magu Mwanza.

June 2, 2023 La Ezekiel Charle Pamoja Na Wenzake Wawili Wamefikishwa Katika Mahakama Hii Kwa Kosa La Mauaji Na Ushirikina.

Watu Hao Wamefikishwa Katika Mahakama ya wilaya ya Magu Kwa Kosa La Mauaji Ya Mwanamke Aliyejuliakana Kwa Jina La Esther Lukoni Ambaye Walimkata Sehemu Zake Za Siri Kisha Kuzikausha Kwa Ajili Ya Kuchanganya Kwenye Dawa.

Washtakiwa Waliofikishwa Mahakamani Ni Pamoja Na Masunga Mabula Mwenye (32), Ezekiel Charles (40) na Salome Raphael (32), Wakisomewa Shtaka Lao Mbele Ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Wa Mahakama Ya Wilaya Ya Magu Amani Mahimba Wamesomewa Kesi Ya Mauaji Namba Sita Ya Mwaka 2023

Akisoma Shtaka Hilo La Mauaji Linalowakabili watatu hao Mwendesha Mashtaka Wa Serikali Mkaguzi Msaidizi Wa Polisi Chacha Msenye Amesema Mnamo mei 19 Mwaka Huu Washtakiwa Hao Walitenda Kosa La Mauwaji Ya Mwanamke Esther Lukoni Kwa Kumnyonga Shingo Kisha kumbaka Na Kumkata Sehemu Zake Za Siri Na Mwili Wake Kuutupa Kwenye Shamba La Mihogo

Washtakiwa Hao Wametenda Kosa Hilo Kinyume Na Kifungu Namba 196 Na 197 Cha Sheria Ya Kanuni Ya Adhabu Sura Ya 16 Marejeo Ya Mwaka 2022. Mara Baada Ya Kusomewa Shtaka Hilo Washtakiwa Wote Hawakutakiwa Kujibu Chochote Kutokana Na Mahakama Hiyo Kutokuwa Na Uwezo Wa Kusikiliza Shtaka La Mauaji Na Kurudhishwa Rumande Katika Gereza La Wilaya Ya Magu Hadi Tarehe 16 juni mwaka huu Hadi Kesi Hiyo Itakapotajwa Tena

Leave A Reply