The House of Favourite Newspapers

Angelina Jolie Aomba talaka

angelina-jolie-1Angelina na Brad Pitt.angelina-jolie-3Angelina na Brad Pitt enzi penzi lao likiwa moto.

MAREKANI: Mwanadada gumzo kwenye ulimwengu wa uigizaji kutoka Hollywood nchini Marekani, Angelina Jolie (41) ameomba talaka ya kuachana na bwana wake ambaye pia ni muigizaji maarufu nchini marekani na duniani kwa ujumla Brad Pitt.

mwanadada huyo ameomba kuachana na bwana wake huyo huku chanzo kikubwa kikitajwa kama kitendo cha Brad Pitt kuwabagua watoto wa Angelina aliowazaa kabla ya kuolewa na Brad Pitt.

Pia chanzo kingine kinataja sababu kuu ya Angelina kuomba kuachana na mumewe huyo waliyedumu naye kwa miaka 12 kuwa ni fununu za Brad Pitt kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Marion Cotillard.

Kupitia mtandao wa DailyMail.com Brad Pitt amesema:
“Nimeshtushwa sana na tukio hili la Angelina kuomba talaka, lakini jambo muhimu kwa sasa ni kuwaangalia watoto wetu na hatma yao.”

Comments are closed.