The House of Favourite Newspapers

Anna Maboya Corona Imetibua Mipango Ya Kuitangaza Injili Kimataifa

0

PIGO la Virusi vya Corona halijaigusa familia ya michezo peke yake hapana kila sekta imeguswa na kuvurugwa kwa namna inavyotaka na kuacha maumivu pia.Kwa upande wa injili pia mambo yamekuwa tofauti na mwanzo ambapo ibada zimekuwa na mpangilio tofauti ikiwa ni tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona ambavyo bado ni janga la dunia vikisababisha Ugonjwa wa Covid-19.

 

Anna Maboya ni mwimbaji wa nyimbo za injili ambaye alikuwa kwenye mpango wa kuachia albamu yake mpya kabla ya mwezi Machi, mwaka huu ila ghafl a Corona ikatibua mipango yote na kuiacha iende kwa namna nyingine ya tofauti.

Wimbo wake wa The Battle is Not Yours aliouachia Novemba Mosi, 2019 ni miongoni mwa kazi ambazo zinafanya vema na tayari mkononi alikuwa na mialiko kutoka nje ya nchi pamoja na ile ya ndani lakini sasa hili janga limetibua kila kitu.

Mbali na wimbo huo pia alikuwa na nyimbo nyingine ambazo zilikuwa zinafanya vizuri ikiwa ni pamoja na Sifa na Hakuna Usiloliweza pia.Championi Ijumaa limefanya mahojiano na mwimbaji huyo ambaye alihojiwa na kituo cha redio cha +255 Global Radio, amefunguka mengi.

+255 Global Radio ambayo ipo hewani saa 24 kila siku, inasikika kupitia Application inayopatikana Playstore na AppStore katika Android na iOS kwa kuandika 255globalradio.Pia unaweza kutembelea tovuti ya www.globalradio.co.tz/ ambapo utapata habari, picha na video mbalimbali kisha utasikiliza redio ukiwa na bando kiduchu tu.“Katika hili ambalo tunapitia kwa sasa tunapaswa tuendelee kumuomba Mungu ili hali iwe salama kwani njia ya kutoka ipo na tunayemtegemea ni mkubwa katika hili tutapita bila mashaka,” anaanza kutiririka Anna Maboya na kuendelea.

anna

UNADHANI KIPI AMBACHO KINAWATESA WATU?“Kikubwa ambacho kwa sasa kipo kwenye mioyo ya watu ni hofu ambayo inatuponza na inatufanya tushindwe kufi kia malengo kwani inakata ile nguvu ya kujiamini na nguvu ya kushinda. Lazima tuishinde hofu ili tuibuke washindi. Pia inapunguza kinga ndani ya mwili pale inapozidi.

 

KIIMANI CORONA INAMAANISHA NINI?“Corona ninavyojua mimi ukiachana kwamba ni janga la dunia, ninaelewa kuwa ni adui ambaye ameletwa kuvuruga mambo katika mipango ambayo tunayo, kwa kuwa Mungu wetu hashindwi, huyu adui tutamshinda.

 

UNADHANI KWA NINI HAYA YANATOKEA?“Vita si yetu ni ya bwana, ni miongoni pia mwa kazi zangu ambazo niliwahi kuimba. Ila hii inatokea ili iwe fundisho, kuna wakati tunapitishwa mahali ili kuweza kufi kia kule ambako anahitaji twende kwani anaendelea kutuimarisha na kutufanya tuzidi kuwa imara ni yeye bwana anajua.

 

TUNATAKIWA KUFANYA NINI?

“Wajibu wetu ni kuendelea kuomba mpaka pale tunachokitaka kitokee, haja yetu Mungu anaijua kwa imani inawezekana, tumuombe yeye bila kuchoka.“Jukumu letu ni moja kuomba bila kuchoka na kushukuru pia kwani tumeambiwa tumshukuru bwana kwa kila jambo.

 

KWA SASA MIPANGO INAKWENDAJE?

“Awali nilikuwa kwenye mpango wa kuzindua albamu yangu mpya pamoja na ziara za ndani na nje ya nchi. Sasa baada ya janga la Corona kwa sasa hakuna kinachoendelea kwani mambo yamesimama.“Kulikuwa na kazi za kufanya kimataifa pamoja na ziara kwenye makanisa mbalimbali kwa ajili ya kumtukuza Mungu, maandalizi ya matamasha nayo yote ilinibidi niyakatishe ghafl a ila ninashukuru Mungu anatupigania bado tunaendelea kupambana.

 

KWA SASA IBADA ZIPOJE?

“Kuna mabadiliko tofauti na ilivyokuwa awali ambapo kulikuwa na uhuru kwa waumini kukaa karibu na kusifu pamoja ila zinaendeshwa kwa kuzingatia kanuni. Waumini wanakaa umbali wa mita moja ili kupeana nafasi pia kila muumini anayeingia na kutoka ananawa kwa maji tiririka.

 

UJIO WAKO WA ALBAMU JE UPOJE?

“Kwa kweli acha kwanza hili lipite ndipo nitapata utulivu wa kuanza kufi kiria tena masuala ya albamu kwa sababu tayari mpango ulikuwa umekamilika ila hili janga.“Nina amini kila kitu kitakuwa sawa kwa sasa dunia nzima ipo kwenye maombi kuhusu hili suala na hata Rais John Magufuli anasisitiza watu kuomba amekuwa kiongozi wa kipekee tuzidi kushikamana Watanzania na dunia nzima kiujumla ushindi upo.”

Makala-Bongo: LUNYAMADZO MLYUKA

Leave A Reply