The House of Favourite Newspapers
gunners X

Anne Makinda: Sikustahili Kuwa Spika, Niliazima Nguo ya Kuapishwa – Video

0

SPIKA wa mstaafu wa bunge, Anne Makinda, amelieleza bunge jinsi alivyoazima nguo kwa ajili ya kuapishwa ubunge kwa mara ya kwanza mwaka 1975. Makinda amekuwa mbunge kwa miaka 40.

 

Amesema hayo jana Jumanne, Januari 28, 2020,  wakati akilishukuru Bunge kwa kutambua mchango wao (maspika wastaafu) na kuwapa heshima ya kuvaa vazi la uspika ndani ya bunge katika mkutano wa 18 bunge la 11.

 

Akizungumzia namna alivyoingia bungeni,  amesema kuwa alifika bungeni hapo akiwa mdogo bila hata kujua mavazi anayostahili kuvaa.

 

“Wabunge wote duniani hata wakipigana ndani ya bunge lakini uzalendo kwa nchi yao ni mkubwa, huwezi kukuta Mmarekani anaizungumzia nchi yake ovyo, huwezi mbunge ukazungumza vibaya kuhusu nchi yako, tofauti zetu za itikadi zisitugawe sisi ni Watanzania,” alisema.

 

Alisema  tofauti za itikadi zisiwagawe wabunge na wananchi kwani wote ni Watanzania na kwamba mfumo wa vyama vingi ulianzishwa na wabunge wenyewe hivyo ni sheria kuwa na vyama vingi na havimaanishi kuigawa nchi.

 

“Na sisi kama tukitaka kujenga nchi hii uzalendo lazima kiwe kitu cha kwanza kwa sababu nchi hii ni ya kwetu sisi wote, tofauti zetu za itikadi zisitugawe sisi ni Watanzania.  Hata kuwe na vyama vingi, kama tunavyosema sheria ilianzishwa na bunge hili.  Ni sheria si kwamba ni hiari; ni sheria kuwa na vyama vingi.  Ni sheria kwani tuliipitisha sisi wenyewe hapa” alisema.

 

Pia, amesisitiza juu ya unyenyekevu ambao wabunge wanatakiwa kuwa nao kwa wananchi wao ambao wanautumia kama daraja kufikisha shida zao ili ziweze kutatuliwa.  Hivyo amewaomba waendelee kuwa wanyenyekevu ili wananchi wawe huru kufikisha shida zao kwao.

 

Ameongezea kuwa mbunge yeyote ambaye siyo mnyenyekevu kwa wananchi wake ni mbunge mwenye mashaka. Aidha amewaasa wabunge kuendelea kujifunza kila siku kwa wazee waliowatangulia na amewataka kuwa wazalendo kila siku kwa ajili ya nchi yao.

 

Leave A Reply