The House of Favourite Newspapers

Anti Lulu akiri bwana wake kubwia unga

auntlulu1DAR ES SALAAM: Msanii wa filamu aliyekuwa akipiga dili la utangazaji, Lulu Semagongo ‘Anti Lulu’ baada ya kudaiwa kuwa anatumia unga, ameibuka na kukanusha madai hayo ila akakiri kuwa anayetumia ni bwana’ke, ndio maana watu wanasema naye anatumia.

Akipiga stori na Ijumaa, Anti Lulu alifunguka mazito na kudai kuwa watu wanamzushia mengi sana kwa sababu amebadilika na wengi humpigia simu wakimtajia mpaka pesa ili arudi kwenye mambo hayo ya kidunia lakini amekuwa akiwakatalia.

Msikie

“Da! Unajua mimi nashangaa kuzisikia hizo habari, hata familia yangu iliniita na kuniweka kikao kizito wakidai kwamba nipo na mwanaume anayevuta unga nami nimeanza kutumia lakini nikawahakikishia kuwa siwezi kuvuta kwa sababu nilikotoka kwa marafiki na kampani mbalimbali za watu waliokuwa wakivuta sana unga lakini nimeokoka nashukuru Mungu.

“Kuvuta ni akili ya mtu wakati mwingine maana ningekuwa nishavuta siku nyingi.”

 aunt lulu

Hakujua kama bwana’ke anavuta

“Wakati naanza uhusiano na bwana’angu sikujua kama anavuta, niliposikia maneno sana kwa watu nilimbana ndiyo akanieleza kuwa kweli anavuta lakini tangu nijue nimekuwa naye bega kwa bega kuhakikisha anaacha.”

Aongelea maisha yake

“Maisha yangu sasa hivi yamebadilika sana, nimekuwa mtu wa Mungu nimeachana na marafiki wasiokuwa na maendeleo ndiyo maana muda mwingi nipo kwa mama.”

Anasali kwa Suguye

“Kutokana na mambo ya kidunia kutonisaidia, nimeamua kusali kwa mchungaji Suguye maeneo ya  Matembele Yapili, Kivule, Dar ikiwa ni baada ya kuguswa na mahubiri yake kwenye runinga nikaamua kwenda kanisani hapo.

“Mpaka sasa nishaenda mara mbili kwani nilianza rasmi Januari Mosi, mwaka huu na kila nikienda somo linaniingia hivyo hata pombe nimeacha namshukuru Mungu.”

Azungumzia kazi 

“Nina project kubwa nimepata na ndiyo maana ninajipanga, nimepumzika kuuweka mwili sawa nitatoka na kitu cha tofauti kwenye hiihii fani yangu ya utangazaji mashabiki wangu wakae mkao wa kula.

“Watu wamenisema sana, wapo wanaodhani nimekwisha, si mmeniona jamani bado ni Anti yuleyule, tena ninalipa ni jambo la kushukuru, kwa kweli Mungu asifiwe sana,” alimaliza Anti Lulu.

Comments are closed.