The House of Favourite Newspapers

Anyongwa Hadi Kufa kwa Kukutwa na Misokoto 14 ya Bangi!

chijioke-obioha

Singapore: Mwanamme mmoja raia wa Nigeria amenyongwa hadi kufa nchini Singapore kwa kuhusika kwenye ulanguzi wa Madawa ya Kulevya baada ya kupatikana na kilo 2.6 za bangi.

Mwanamme huyo Chijioke Stephen Obioha mwenye miaka 38, alinyongwa jana Novemba 18, 2016 katika Gereza la Changi.

Obioha ambaye ana shahada ya kemia ya viwanda kutoka Chuo cha Benin, alihamia nchini Singapore mwaka 2005, akiwa na matumaini ya kuwa mawanasoka.

Alikamatwa mwaka 2007 wakati alipatikana na misokoto 14 ya bangi ndani ya mkoba wake, na misokoto mingine 14 kweye nyumba alimokuwa akiishi. Alipatikana na hatia ya kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa mnamo Desemba 2008, licha ya kukata rufaa mwaka 2010 ambayo pia alishindwa.

Shirika la Haki za binadamu Duniani (Amnesty International) limefanya kila jitihada kunusuru uhai wa Obioha kwa kuwashauri wakuu wa magereza na serikali ya Singapore wasimtie kitanzi lakini haikuwezekana. Shirika hilo limeeleza kuwa kunyonga watuhumiwa wa madawa ya kulevya siyo njia sahihi ya kukomesha tatizo la madawa hayo nchini Singapore.

Chini ya sheria za Singapore, mtu yeyote ambaye atapatikana akiwa na zaidi ya gramu 500 za bangi anaweza kuhukumiwa kifo.

Chanzo: Strait Times

halotel-strip-1

Comments are closed.