Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Kampasi ya DUCE, jana walifanya tamasha la kuonyesha vipaji mbalimbali ikiwemo mitindo ya mavazi, uchoraji, kucheza, kuimba na mambo mengine.
Pamoja na hayo pia ilizulinduliwa APP ya Global Publishers chuoni hapo ambapo wanafunzi hao walishauriwa kujiunga na APP hiyo ili wawe wa kwanza kupata matukio mbalimbali yanayojiri hapa nchini na ulimwenguni, interviews za mastaa, burudani, michezo, vitabu vya Eric Shigongo katika mfumo wa maandishi (text) na sauti (audio).
Akizungumza na wanachuo hao, mwakilishi wa Global Publishers, Snash Sekidia, aliwaambia wajiunge na APP hiyo ili kuwa miongoni mwa wafuatiliaji zaidi ya milioni tatu wanaoifuatilia Global APP kila siku ambapo Jumatatu ijayo, litaanza shindano kwa wnaopakua Global App watajishindia tablets na bundles za internet.
Katika tamasha hilo wanachuo hao walishindana kuonyesha vipaji mbalimbali na kukonga nyoyo za watazamaji waliokuwa wakilipuka kwa mayowe ya kushangilia.
Sambamba na tamasha hilo Mkufunzi wa Ujasiriamali, James Mwang’amba, naye aliwapa somo la ujasiriamali wanachuo hao ambalo lilivuta hisia zao kwa kiwango kikubwa.
Install #GlobalPublishersApp hapa
Android: ==>bit.ly/2AAQe1d
iOS: ==> apple.co/2Assf4M
HABARI/ PICHA: RICHARD BUKOS / GPL
Comments are closed.