APP YA GLOBAL YAZINDULIWA KAMPASI YA DUCE CHUO KIKUU DAR – VIDEO

Wanachuo  wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Kampasi ya DUCE wakifanya ‘machejo’ mbalimbali wakati wa tamasha la kuonyesha vipaji.

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Kampasi ya DUCE, jana walifanya tamasha la kuonyesha vipaji mbalimbali ikiwemo mitindo ya mavazi, uchoraji, kucheza, kuimba na mambo mengine. 

Mwanafunzi akionyesha kipaji cha uchoraji.

Pamoja na hayo pia ilizulinduliwa APP ya Global Publishers chuoni hapo ambapo wanafunzi hao walishauriwa kujiunga na APP hiyo ili wawe wa kwanza kupata matukio mbalimbali yanayojiri hapa nchini na ulimwenguni, interviews za mastaa, burudani, michezo, vitabu vya Eric Shigongo katika mfumo wa maandishi (text) na sauti (audio).

 

Mawaziri wa chuo hicho (waliokaa mstari wa mbele) na wanachuo wengine wakifuatilia mashindano hayo.

Akizungumza na wanachuo hao, mwakilishi wa Global Publishers, Snash Sekidia, aliwaambia wajiunge na APP hiyo ili kuwa miongoni mwa wafuatiliaji zaidi ya milioni tatu wanaoifuatilia Global APP kila siku ambapo Jumatatu ijayo, litaanza shindano kwa wnaopakua Global App watajishindia tablets na bundles za internet.

Mkufunzi wa Ujasiriamali, James Mwang’amba, akitoa somo la ujasiriamali kwenye tamasha hilo.

Katika tamasha hilo wanachuo hao walishindana kuonyesha vipaji mbalimbali na kukonga nyoyo za watazamaji waliokuwa wakilipuka kwa mayowe ya kushangilia.

Mwakilishi wa Global Publishers kwenye tamasha hilo, Snash Sekidia, akiwaeleza wanachuo umuhimu wa kujisajili kwenye APP ya Global Publishers.

Sambamba na tamasha hilo Mkufunzi wa Ujasiriamali, James Mwang’amba, naye aliwapa somo la ujasiriamali wanachuo hao ambalo lilivuta hisia zao kwa kiwango kikubwa.

Baadhi ya washindi waliwa na zawadi zao. 

 

Wakati wa kutunukiwa zawadi. 

Install hapa

Android: ==>

iOS: ==>

HABARI/ PICHA: RICHARD BUKOS / GPL  

Wanachuo DUCE Washindana Kuonesha Vipaji, Global APP Yawa Gumzo 


Loading...

Toa comment