The House of Favourite Newspapers

Archbishop Anthony Mayala Girls Secondary School

0

Mkombozi wa wasichana waliokata  tamaa ya kuendelea na masomo

bishop-schoolNa Idd Mumba, Mwanza

SHULE mpya ya sekondari ya Archbishop Girls iliyopo katika Kijiji cha Ibindo wilayani Kwimba mkoani Mwanza ikiwa chini ya Parokia ya Nyambiti, ni maalum kwa ajili ya wasichana waliopata ujauzito shuleni wakiwa na umri mdogo, kitu kilichowafanya wakose kuendelea na masomo.

Wengi waliokutana na hali hiyo wamejikuta wakikata tamaa ya kupata elimu ya sekondari na hivyo kukata tamaa ya maisha yao ya baadaye.

Wazo la kuanzishwa shule hiyo

Katika kila mafanikio ambayo mtu huyapata, hutokana na wazo linalomfanya ajifikirie na baadaye kupambana na changamoto zinazomkabili kama ilivyomtokea Padri Ibrahim Ngassa Joseph.

Baada ya kupadrishwa Agosti 30, 2009 wasichana wengi walijitokeza kuomba malipizi ili kujipatanisha na Kanisa Kisakramenti. Kutokana na idadi yao kuwa kubwa ilimfanya kutambua kuwa jamii inayomzunguka inakabiliwa na tatizo kubwa la wasichana kupata mimba za utoto na kutelekezwa, wengi wao wakishindwa kuendelea na masomo ya sekondari.

Baada ya kupata wazo hilo, Padri Ngassa aliamua kulifanyia kazi kwa kuanzisha shule hiyo mwaka 2010 ikiwa na wanafunzi 63, wote wakiwa ni wasichana wenye watoto mmoja mmoja na 6 wakiwa tayari wana watoto wawili, wakitokea Wilaya za Kwimba na Shinyanga Vijijini.

Ugumu uliojitokeza

Katika mafanikio yoyote, jitihada zinahitajika ili kukabiliana na changamoto zinazozuia kufikia malengo na mafanikio. Awali, shule hiyo ilianza kama ya kutwa (Day), wanafunzi wakitoka majumbani kwao na wengine wakiwa wamepanga vyumba (geto), kitu kilichowafanya waanze kujiingiza katika uhusiano wa kimapenzi kutokana na kutokuwa na ulinzi wa kutosha.

Jambo hili lilimfanya padri huyo kuzidisha bidii katika kutafuta michango kutoka kwa waumini na watu mbalimbali ili kujenga mabweni kwa ajili ya wanafunzi hao.

Penye nia pana njia kwani michango na harambee za  wanakijiji na wadau wengine, walifanikiwa kujenga mabweni hayo, huku mchango mkubwa ukitoka Kampuni ya Global Publishers, wachapishaji wa Magazeti ya Championi, Risasi, Ijumaa, Amani, Uwazi na Uwazi Mizengwe, kiasi cha kuwafanya wanafunzi kupata  huduma zote wakiwa shuleni.

Mafanikio yaanza kuonekana

Mafaniko ya shule hiyo yalianza kuonekana baada ya wanafunzi hao kufanya mtihani wa kidato cha pili mwaka 2013 na kushika nafasi ya kwanza katika Wilaya ya Kwimba na nafasi ya 37 Mikoa ya Kanda ya Ziwa. Idadi ya wanafunzi pia iliongezeka hadi kufikia 93 kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne na mwaka huo huo watahiniwa 31 wa kidato cha nne walifanya mtihani wa kuhitimu na 19 kati yao, wakafanikiwa kujiunga na kidato cha tano.

Mwaka uliofuata (2014), wahitimu walikuwa 38  wa kidato cha nne na 31 wakafanikiwa kufaulu na kujiunga na kidato cha tano na mwaka huu watahiniwa 42 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kidato cha nne.

Falsafa ya shule

Shule inawalea wanafunzi kwa kufuata falsafa ya aliyekuwa Askofu Anthony Petro Mayala, aliyeamini katika Ukweli, Unyenyekevu na Ukarimu. Pia aliamini katika umaskini wa watu, matendo makuu ya Mungu hudhihirika.

Kutokana na falsafa hiyo, shule inawasaidia wasichana wa makabila, dini na madhehebu yote waliokosa nafasi ya kuendelea na masomo kutokana na kupata ujauzito wakiwa na umri mdogo. Shule inapokea wanafunzi wote wa kike ilimradi awe tayari kufuata malezi na maisha ya seminari yaani (kusali, nidhamu bora, utii kwa watu wote, kusoma kwa bidii, kufanya kazi kwa ushirikiano na wanafunzi wenzake pamoja na kushiriki shughuli mbalimbali za pamoja.

Michepuo inayofundishwa

Shule inafundisha michepuo ya sayansi kwani tayari ina maabara nne za Physics, Chemistry, Biology na Geography, michezo mbalimbali, ngoma za asili za utamaduni wa Kitanzania pamoja na stadi za maisha kama ujasiriamali, kute      ngeneza sanaa za mikono, uigizaji na kuibua vipaji mbalimbali kwa wanafunzi na kuviendeleza ili kufikia malengo yao.

Mazingira ya shule

Mazingira ya shule yanamruhusu mwanafunzi kusoma kwa bidii kutokana na kupatiwa huduma nzuri zinazostahiki, eneo la kutosha kwa michezo na mapumziko.

JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS!

globalbreakingnews.JPG

Leave A Reply