The House of Favourite Newspapers

Argentina Yaanza Vibaya Kombe la Dunia, Yaambulia Kichapo Kutoka kwa Saudi Arabia

0
Nahodha wa Argentina Lionel Messi akishangilia bao alilofunga dhidi ya Saudi Arabia kwa njia ya mkwaju wa penati

TIMU ya Taifa ya Argentina inayoongozwa na nyota na moja ya wachezaji bora duniani wa muda wote Lionel Messi imeanza vibaya mashindano ya fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar kwa kuambulia kichapo cha bao 2-1 dhidi ya Timu ya Taifa ya Saudi Arabia.

 

Argentina ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia mkwaju wa penati uliowekwa kimiani na nahodha wa timu hiyi Lionel Messi hadi mapumziko Argentina ilikuwa inaongoza kwa bao 1-0.

 

Kipindi cha pili Saudi Arabia walicheza mchezo wa kushambulia kwa kushtukiza pamoja na kucheza mtindo wa kutegea kuotea (Offside Trick) na kufanikiwa kupata mabao mawili yaliyofungwa na Al-Shehir katika dakika ya 49 pamoja na AlDawsari katika dakika ya 53.

Wachezaji wa Saudi Arabia wakishangilia bao walilofunga dhidi ya Argentina

Katika mchezo huo jumla ya wachezaji sita (6) wa Saudi Arabia walipewa kadi za njano huku Argentina ikiwa haijapewa kadi hata moja.

 

Kwa matokeo hayo Saudi Arabia inaongoza kundi ikiwa na jumla ya alama 3 huku Argentina ikiburuza mkia kwa kuwa na point 0 ikiwa imebakiwa na michezo miwili.

Leave A Reply