Ariana Aionyesha Pete ya 228bn ya Uchumba ya Pete Davidson

HATIMAYE  baada ya kuyaonyesha mapenzi yao wazi na kimwana wake,  Pete Davidson kamvisha mchumba’ke, Ariana Grande, pete ya thamani ya Dola 100,000 ambazo ni sawa na Sh. 228m ambapo pia alilipa Sh. 212m katika kugharamia hafla ya uvishanaji wa pete hiyo aliyoinunua mwezi uliopita.

Pete hiyo ya mtindo wa VVS1 ikiwa na ‘carat’  3.03 za almasi, ilitengenezwa na muuza vito wa New York aitwaye Greg Yuna, ambaye anafahamika pia kama Mr. Flawless. Inasemekana ilichukua karibu wiki mbili kuikamilisha pete hiyo.

Mashabiki wamesema kwamba Ariana ambaye ni mwimbaji wa wimbo wa  “No Tears Left to Cry” amekuwa akitumbuiza jukwaani akiwa na pete hiyo tangu Juni 2 mwaka huu alipokuwa katika onyesho la  KIIS FM’s Wango Tango. Alionekana pia akiwa ameivaa katika onyesho la Kanye West na  Kid Cudi la Kids See Ghosts wiki iliyopita.

Baada ya habari za kuchumbiana kwao kufahamika, Grande alithibitisha hilo kwenye akaunti zake za mitandao kwa ujumbe mbalimbali akijibu hoja mbalimbali za mashabiki wake.

Wanandoa hao watarajiwa  walitembelea eneo la burudani la Disneyland ambako mashabiki wao waliwaona na kuwafurahia.

Pete na Ariana wamechumbiana baada ya kuwa na uhusiano wa muda mfupi.  Ariana aliachana na mpenzi wake, Mac Miller, mwanzoni mwa mwaka huu, wakati Davidson aliachana na binti wa Larry David aitwaye Cazzie.

 

Loading...

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment