The House of Favourite Newspapers

Ariana, Davidson Wahamia Makazi Mapya New York

Pete na Ariana.

WACHUMBA ambao ni wasanii maarufu nchini Marekani, Ariana Grande na  Pete Davidson wamehamia katika makazi mapya jijini New York eneo la Manhattan jirani na kitongoji cha Chelsea ambako makazi hayo yana thamani ya karibu Sh. bil. 40 (Dola  mil. 16), makazi ambayo yamepambizwa kwa usanii wa mtaalam wa mapambano,  Zaha Hadid.

Makazi hayo ambayo yana nafasi kubwa ya uwanja, vitanda vitano na maliwato matano, bwawa la kuogelea na kadhalika, yako kwenye eneo lenye kuweza kuona mandhari za sehemu kubwa ya jiji hilo.

 

Makazi mapya ya Ariana na Pete.

Haijafahamika iwapo wapenzi hao wameyanunua makazi hayo au wamepanga tu, lakini kutokana na tetesi zilizopo, hayo ni makazi ambayo ni mali yao.

Comments are closed.