The House of Favourite Newspapers

Ariana Grande Apigwa Pete ya Uchumba

0

KILA mwaka huwa na matukio yake ya kihistoria yanayojiri.  Mwaka 2020 umeleta makubwa mengi  bila kusahau janga la ugonjwa wa Covid-19 na mengineyo, lakini yote hayo hayajaweza kusimamisha jambo liitwalo penzi. Tumeshudia tayari ndoa nyingi za watu maarufu zikifungwa mwaka huu.

Sambamba na hilo, msanii #ArianaGrande kutoka nchini Marekani pamoja na mchumba wake, Dalton Gomez, ambaye ni mfanyabiashara mkubwa wa Real Estate, wamemaliza mwaka kwa kuvishana pete ya uchumba. Pete hiyo ya #Ariana inatajwa kuwa imetengenezwa kwa madini ya almasi.

 

Aidha, tovuti ya ‘People’ inaripoti kwamba wawili hao walianza kuwa kwenye mahusiano tangu mwezi Januari mwaka huu.

Hata hivyo, tangu TMZ kuleta habari hii kivingine mwezi Mei (kwa uthibitisho wa picha za wawili hao wakiwa mgahawani) ndipo watu wengi walianza kuelewa uwepo wa penzi jipya mjini. Hilo lilipelekea #Ariana aanze kumpost #Gomez mara kadhaa kwenye ukurasa wake wa Instagram.

 

Hii si mara ya kwanza kwa #Ariana kuvalishwa pete ya uchumba, mwaka 2018 pia alivalishwa pete na aliyekuwa mpenzi wake wa kipindi hicho #PeteDavidson na penzi lao likavunjika baada ya mwaka mmoja.

Leave A Reply