ARISTOTE AFUNGUKIA BIFU LAKE NA UWOYA

Aris Mwamtobe ‘Aristote’

SIKU chache baada ya habari kusambaa mitandaoni kuwa ana bifu kali na msanii wa filamu Bongo, Irene Uwoya huku chanzo kikidaiwa amekuwa akimsifia sana mpenzi mpya wa Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’, mpambaji maarufu wa wasanii wa kike, Aris Mwamtobe ‘Aristote’ ameibuka na kufungukia tofauti zao.  

 

Awali ilidaiwa kuwa, Uwoya ambaye alikuwa mteja mzuri wa saluni ya Aristote walikuwa kwenye bifu kali huku baadhi ya mashabiki wakimpa jina lingine Aristote la Yuda Msaliti ikiwa ni baada ya video kusambaa mitandaoni akimsifia mpenzi mpya wa Dogo Janja ambaye alikuwa mume wa staa huyo wa filamu.

 

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Aristote alisema hana tatizo lolote na Uwoya kwa sababu alichokiongea kwenye video iliyosambaa ni kweli licha ya kwamba tangu iliposambaa msanii huyo hajafika tena kwenye saluni yake wakati ndiye staa aliyekuwa akitoa mkwanja mrefu kwa kujipamba.

 

“Kiukweli sijisikii vizuri kabisa kupewa hayo majina (Yuda na mnafiki) nina watoto wanakua kesho wakisikia baba yenu alikuwa anaitwa Yuda yaani msaliti inakuwa haileti maana nzuri kabisa, lakini tangu hayo maneno yasambae mitandaoni hajawahi kuja hapa ofisini kwangu, zaidi ya kukutana naye tu mara moja.

“Pia isitoshe hii hainipunguzii kitu chochote kwa sababu naamini Uwoya siyo mtu wa kukaa na kinyongo muda mrefu, pia tatizo kubwa ni hawa wapambe ndiyo wanaomjaza maneno lakini yeye mwenyewe hana tatizo na mtu, ingawa mchumba wa Dogo Janja akija tena kutengeneza nywele dukani kwangu nitamsifia kama kawaida na Uwoya naye akija nitafanya hivyohivyo,” alisema Aristote.

 

Mpambaji huyo amejizolea umaarufu baada ya kuonekana akiwapamba mastaa wengi Bongo akiwemo Elizabeth Michael ‘Lulu’, Jacqueline Wolper, Rita Paulsen ‘Madam Ritha’ na wengineo huku akichombeza kwa kutaja maneno tofautofauti ya kuchekesha akiambatanisha na jina la ‘Aristoste mzee wa vikao’.

STORI: Memorise Richard, Dar es Salaam

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Toa comment