Aristote: Lulu Kanifanya Nijulikane, Wema Anaogopa Kuja Kwangu

 

Aris Mwamtobe ‘Aristote’.

MPAMBAJI Aris Mwamtobe ‘Aristote’ amejitengenezea jina kwa kupamba watu maarufu Bongo.

 

Aristote amekuwa akiwapamba mastaa mbalimbali kama IreneUwoya, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Hamisa Mobeto,Natashampenzi wa Diamond Platnumzna wengineo kibao.

… Akiwa na Elizabeth Michael ‘Lulu’.

Aristote amekuwa akihusishwa kuwa na skendo yakuwakuwadia wasanii wanaume, kuhusiana na hilo tiririka ujue vitu vingi vyake.

 

Spoti Xtra: Mambo vipi Aristote, nini siri ya mafanikio yako?

… Akiwa na Tanasha.

Aristote: Poa tu, siri ya mafanikio yangu ni kujituma zaidi na kuhakikisha natoa huduma nzuri kwa wateja wangu si unaona nimewawekea mpaka winekwa hiyo huku namtengeneza mteja huku anapata kinywaji baridi.

Spoti Xtra: Ok, hivi Aristote ndio jina lako la kuzaliwa au umeamua kulitumia tu kibiashara?

 

Aristote: Nimeliboresha ili kuliwekea manjonjo tu na kuwavutia watu, jina langu halisi niArisMwamtobe.

…Akiwa na Jokate.

Spoti Xtra: Watu wengi wamekuwa wakikufuatilia kwenye mitandao ya kijamii kutokana kazi nzuri unazofanya, vipi ulianzaje?

 

Aristote: Aristote wa zamani sio wa sasa hivi, nakumbuka nilikuwa nimeajiriwa sehemu tofautitofauti, lakini baadaye nikaja kupata chansi ya kuajiriwa Darling kwenye kiwanda cha nywele, nashukuru Mungu walinikubali nikafanya nao kazi.

Baadae kutokana na ubora wa kazi zangu kuna dada alikuja akaniiba akaahidi kunipa pesa mara mbili ya niliyokuwa napokea kwenye kiwanda cha Darling hivyo nikaenda kufanya kazi kwenye saloon yake Posta.

 

Nilifanya kazi pale kwa muda kidogo, hivyo baadaye akahamishia tena saloon yake Mikocheni tuliendelea kufanya kazi lakini baadaye zikaanza chokochoko za hapa na pale mwisho wa siku yule bosi wangu akaniita akaniambia Aristote kazi basi, ‘kwa sababu nimegundua nikibaki na wewe siku ukiondoka wateja nitakuwa sina, kwa sababu hata ukiwa mapumziko wateja nao hawaji’.

 

Nikaondoka kwa huzuni kwa sababu kwanza nilifukuzwa kazi bila kutegemea, lakini pia nilifukuzwa kazi kipindi ambacho mke wangu alikuwa ndio ametoka kujifungua.

 

Nilirudi nyumbani nikamwelezea mke wangu, nakumbuka alinifariji akaniambia nisijali.

 

Baadaye nikaenda kukodisha saloon karibu na nilipokuwa nafanyia kazi, nilimuomba mmlikina ningemlipa fedha yake baada ya muda f’lani, nashukuru yule dada alikubali.

 

Mungu ni mwema kwani nilipoanza tu kufanya kazi ndani ya miezi miwili wateja walianza kumiminika kama mvua, nikaenda kumlipa mwenye saloon pesa yake kisha nikaendelea na kazi yangu.

 

Hapo sasa ndio mpaka wasanii wakaanza kuja kwa wingi ilifika hatua yule dada ikabidi afunge kwa sababu kuna muda wateja walikuwa wakija pale wanauliza Aristote yuko wapi, yule dada anasema hayupo kwa hiyo nilikuwa nikisikia tu hivyo natoka nje haraka nawaambia nipo, kitendo ambacho kilikuwa kinamuumiza sana.

Mwisho wa siku nilikuja kugundua kuwa ile sehemu niliyokuwa nafanyia kazi ilikuwa ndogo hivyo nikapata wazo la kuja kufungua Kinondoni na nilivyofanya hivyo wale wateja waliokuwa wananisapoti Mikocheni wakaongezeka kama mara kumi hivi.

Spoti Xtra: Kitu gani ambacho huwa unakifanya ili kuwavutia wateja wako?

Aristote: Huwa najitahidi kuboresha kazi yangu, nisizoeleke yaani niende na wakati, kila wakati najaribu kujifunza vitu vipya kutokana na wenzetu wasanii wa nje wanavyofanya, nikiona NickiMinajau Rihannaameweka nywele flani basina miminahakikisha nimefanya hivyo.

Spoti Xtra: Hiki ni kipaji ulichojaaliwa au uliingia darasani ukasomea?

Aristote: Sasa hivi nakiita ni kipaji kwa sababu nimekifanya na nimekipatia kwa kuwa nilikuwa nakipenda, lakini kilichofanya mpaka nikaanza kutengeneza nywele ni ugumu wa maisha, wengine tumefanikiwa kusoma shule ya msingi tu, hatujabahatika kufika chuo hivyo uwezekano wa mimi kupata kazi ulikuwa mgumu, kwa hiyo ikanibidi nijiingize kwenye ujasiriamali ndio nikaingia saloonna hii kazi ndio mkombozi wa maisha yangu.

 

Spoti Xtra: Msanii gani ndiyo amekufanya leo hii kila mtu akujue?

Aristote: Ni Lulu (Elizabeth Michael) amenibrand sana, ametengeneza nywele kwangu kiasi kwamba tukawa marafiki sana, ilifikia hatua hata kama haitaji kutengeneza nywele anakuja tu kupiga stori, kwa hiyo kila alipokuwa akiweka staili ya nywele ina kiki.

Spoti Xtra: Mpaka sasa umewatengeneza wasanii wangapi?

Aristote: Karibia wote hapa Bongo, isipokuwa Wema Sepetu tu.

Risasi: Kwa nini?

Aristote: Mimi nahisi sijamtengeneza kwa sababu kuna baadhi ya wasanii wetu wanakuwaga na bifubifu zao za kikazi, hivyo anahofia labda leo akienda kwa Aristoteanaweza akakutana na flani na sijui wataongea nini wakati hawana mawasiliano mazuri.

 

Si unajua wao wenyewe wanachukuliana mabwana, wanakorofishana kwa hiyo nahisi hicho ndio chanzo kinachomfanya mpaka asije, lakini sio kama hatamani kuja kutengeneza kwangu, ila anaogopa kwa sababu ya hilo.

Spoti Xtra: Kiasi cha chini kabisa kutengeneza nywele kipoje?

Aristote: 10,000 na hii nikuosha tu nywele

Spoti Xtra: Kile cha juu je?

Aristote: Unajua mimi siuzi nywele feki kabisa, huwa nywele zangu nazifuata mwenyewe nje, hivyo siwezi nikasema bei labda uwatafute watu kama kina Uwoya, MadamRitha, Lulu na wengineo ndio wanaweza kukujibu kwa sababu hao ndio mara nyingi wanakuja kutengeneza hapa

 

Spoti Xtra: Tofauti ya kumtengeneza msanii na mtu wa kawaida ipoje?

Aristote: Mimi msanii kwangu ni expensive, namtengeneza msanii kwa bei ya juu tofauti na mtu wa kawaida, kwa sababu nimejijengea mazingira kuwa msanii ana hela, mtu wa kawaida simchaji hela nyingi kwa sababu najua hali ni ngumu na pengine aliweka kwenye kibubu chake mwenyewe ili aje saloon kwangu.

Spoti Xtra: Kuna tetesi kwamba unatabia yakuwachonganisha mastaa ili wasiongee, ni kweli?

Aristote: Ujue kuna wakati mwingine unaweza ukaongea utani lakini mtu akachukulia ‘siriasi’ na akajihisi kuwa unamsema yeye, sina tabia hiyo, ingawa kila mteja anayekuja namsifia kwa wakati wake, ndivyo ninavyofanya kazi na nashukuru kwa sababu hii kazi ndio inasomesha watoto wangu.

Spoti Xtra: Vipi kuhusu kuwakuwadia wasanii wanaume?

Aristote: Siyo kweli, mfano mtu ameona picha au video nzuri ya msanii nimeiposti na yeye hawezi kumfuata huyo msanii kumwambia kuwa amempenda, kwa hiyo ananifuata nakuniambia, kwa hiyo kitu ninachokifanyaga nikufikisha taarifa tu kwa mhusika mambo mengine nawaachia wenyewe.

 

Spoti Xtra: Inasemekana pia hapa saloon kwako wakija watu maarufu ndio unawapa kipaumbele sana kuliko watu wa kawaida, hii imekaaje kwa upande wako?

 

Aristote: Unachokisema kibiashara kiukweli si vizuri, ingawa kuna kitu kinaitwa ‘appointment’, kuna mwingine bado yupo nyumbani anapiga simu kuwa atakuja kusuka muda f’lani hivyo unamuwekea nafasi.

 

Spoti Xtra: Ni mafanikio gani umeyapata tangu umeanza hii kazi?

Aristote: Naishi maisha mazuri sana, pia nimepata mafanikio makubwa mno ingawa bado nazidi kupambana kwa sababu najiona bado sijafikia zile levo ambazo nazitaka.

Spoti Xtra: Inasemekana kwamba ulimpamba Tanasha?

Aristote: Nilipigiwa simu na Diamond akaniambia niende kwake nikampendezeshe mke wake Tanasha, basi nilifanya hivyo na nililipwa vizuri tu.

 

Spoti Xtra: Changamoto zipi unakutana nazo katika kazi yako?

Aristote: Changamoto nyingi ni dharau eti kwa sababu nafanya kazi ya salon, mimi huwa nawaangalia tu kwa sababu hawanijui vizuri.

Spoti Xtra: Hapa saloon wanakuja warembo wengi  na wote wakali, vipi unawezaje kuepuka vishawishi?

Aristote: Vishawishi ni vingi sana kwa sababu kuna wateja wengine wanakuja bila kuvaa nguo ya ndani, hivyo hata akikaa kila kitu kinaonekana wazi, basi unabaki tu kuguna na kujisemea kimoyomoyo kwamba hapa nikicheza vibaya nywele itachukuliwa bure, lakini mwisho wa siku mtu lazima ujiheshimu kwani nina mke na ninamheshimu sana na huwa anakuja hapa saloon.

 

Spoti Xtra: Aristote ni mtu wa aina gani?

Aristote: Aristote ni mtu wa kaiwaida sana, mjasiriamali, mchapakazi, baba wa watoto wawili lakini pia ni mtu anayependa kuongea na kila mtu, ukiishi na mimi vizuri basi na mimi naishi na wewehivyohivyo, ukiniheshimu  na mimi nakuheshimu.

 

Spoti Xtra: Staa gani ambaye huwa anatumia pesa nyingi kutengeneza nywele?

Aristote: IreneUwoya

Spoti Xtra: Uwoya kwa siku anakuja kutengeneza nywele mara ngapi?

Aristote: Uwoyaanabadirisha nywele kila wiki na ni staa pekee naweza nikasema ambaye harudii nywele, akibadilisha nguo anabadilisha na nywele.

Spoti Xtra: Poa asante

MEMORISE RICHARD

 

 

Toa comment