Kartra

Arsenal Kuwakosa Mastaa Watano

ARSENAL huenda ikawakosa nyota wake watano wa kikosi cha kwanza kuelekea mchezo wao dhidi ya Chelsea wikiendi hii.


Awali Arsenal
ilipoteza dhidi ya Brentford ikiwakosa nyota wake wawili wa kikosi cha kwanza Pierre-Emerick Aubameyang na Alexandre Lacazette. Jumapili ya Agosti 22, mwaka huu, Arsenal itakuwa ikivaana na Chelsea katika Uwanja wa Emirates ukiwa ni mchezo wa Premier League.

 

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuna uwezekano baadhi ya wachezaji wakakosekana katika mchezo ujao kutokana matatizo tofauti tofauti.

 

Imeelezwa nyota wengi ambao huenda wakakosekana kwenye mchezo huo ni pamoja na Thomas Partey, Gabriel na Eddie Nketiah pamoja na wale wa awali.

 

Hata hivyo, imeelezwa kufika siku ya mchezo huenda kukawa na mabadiliko ingawa sio kwa asilimia zote. Katika mchezo uliopita, Kocha Mikel Arteta alisema kuwa hatakiwi kuwa na visingizo baada ya kupoteza mchezo wao wa kwanza


Toa comment