The House of Favourite Newspapers

Arsenal Yapigwa EPL na Newcastle United Bao 2-1

Matumaini ya Arsenal kutinga ‘Top Four’ msimu huu wa 2017/18 kwenye Ligi Kuu nchini England (EPL) yanazidi kupotea ambapo leo imekubali kipigo cha goli 2-1 dhidi ya Newcastle United kwenye mchezo wa Ligi Kuu nchini humo.

Kwa sasa Arsenal inahitaji ushindi wa mechi zake tano zilizobakia huku ikiombea klabu ya Chelsea na Spurs kupoteza michezo angalau mitatu ili Arsenal iingie kwenye nafsi nne za juu.

 

Kwa sasa Arsenal wamesalia kwenye nafasi ya sita wakiwa na alama 54 nyuma ya Chelsea alama 60 na Spurs alama 67 na timu zote zina michezo mitano mkononi ya ligi.

Mambo yamekuwa ngumu kwa Arsenal kuliko Chelsea, lakini ahueni kwa Arsenal ni kwamba bado wapo kwenye michuano ya Europa hivyo endapo watashinda taji la michuano hiyo basi kwa sheria mpya watashiriki michuano ya klabu bingwa mwakani moja kwa moja.

Newcastle (4-4-1-1): Dubravka 6.5; Yedlin 6.5, Lejeune 7, Lascelles 6.5, Dummett 6.5; Ritchie 7.5 (Murphy 85), Diame 7, Shelvey 8, Kenedy 6.5; Perez 7.5 (Joselu 79, 6); Gayle 6.5 (Slimani 63, 6)

Subs not used: Darlow, Clark, Hayden, Manquillo

Scorers: Perez 29, Ritchie 68

Manager: Rafa Benitez 7

Arsenal (4-2-3-1): Cech 5; Chambers 5.5 (Maitland-Niles 78, 5), Holding 6, Mustafi 6, Monreal 6; Xhaka 6, Elneny 7; Iwobi 5.5 (Nketiah 86), Willock 5 (Welbeck 68, 5.5), Aubameyang 6.5; Lacazette 6.5

Subs not used: Ospina, Mertesacker, Kolasinac, Nelson

Scorers: Lacazette 14

Manager: Arsene Wenger 6

Comments are closed.