The House of Favourite Newspapers

Arsenal Yataka Kumbadili Lacazette na Jembe la Sevilla

0

ARSENAL wanataka kumbadili mshambuliaji wao Alexandre Lacazette ili wao wampate Youssef En-Nesyri wa Sevilla.

 

Arsenal wanataka kuhakikisha kuwa wanampata staa huyo kwenye usajili wa Januari mwakani na wanaamini kuwa anaweza kuwasaidia kutwaa ubingwa msimu huu.

 

Kocha Mikel Arteta hana mpango na Lacazette na anaamini kuwa anaweza kumtumia vyema kumpata mshambuliaji huyo mwenye uwezo wa hali ya juu uwanjani.

 

Mwishoni mwa msimu huu Lacazette atakuwa amemaliza mkataba wake na Arsenal na inaonekana kuwa timu hiyo haina mpango wa kumuongezea mwingine.

 

Arsenal wanataka kuhakikisha kuwa wanamuondoa klabuni hapo Januari ili kuepuka kumuacha aondoke bure mwishoni mwa msimu huu.

 

Hata hivyo, mashabiki wengi wa Arsenal wamekuwa wakipinga suala la kuondoka kwa mshambuliaji huyo kwa kuwa amekuwa kipenzi chao cha muda mrefu.

LONDON, England

Leave A Reply