The House of Favourite Newspapers

ARSENAL YATANGAZA KUMRUDISHA SUAREZ

Denis Suarez

Arsenal ilimchukua mchezaji huyo kwa mkopo kutoka Barcelona na ameshindwa kuonyesha uwezo wa juu chini ya kocha Unai Emary.

 

Wakati akisajiliwa na timu hiyo, mashabiki walikuwa na imani kuwa anaweza kuitumikia kwa nguvu kwa kuwa alikuwa hajapata nafasi kwenye timu ya Barcelona msimu mzima.

Hadi sasa mchezaji huyo aliyejiunga na Arsenal kwenye usajili wa Januari mwaka huu hajafanikiwa kuanza kwenye mchezo hata mmoja.

 

Taarifa kutoka Arsenal inasema kuwa kocha wa timu hiyo ameamuru mchezaji huyo arudishwe mwishoni mwa msimu na Barcelona watalazimika kumuuza moja kwa moja kwenye timu nyingine kwa kuwa hana nafasi kwenye timu hiyo.

 

Kocha Unai, amesema anataka kumchukua kiungo wa PSG, Christopher Nkunku au yule wa Rennes, Ismaila Sarr, kwenye usajili wa majira ya joto.

Comments are closed.