The House of Favourite Newspapers

Arsenal Yatuma Ofa kwa Winga wa Villarreal, Ana Mkataba Wenye Kipengele Kigumu

0
Yeremy Pina

KLABU ya Arsenal imetuma ofa ya Paundi milioni 40 kwa Villarreal ya nchini Hispania kwa ajili ya kuinasa saini ya winga wa klabu hiyo Yeremy Pino.

 

Mchezaji huyo ambaye pesa yake ya kuvunja mkataba ni paundi milioni 80, pia ameripotiwa kuwa kwenye rada za Liverpool ambao nao wanatarajiwa kutuma ofa ya kumnasa winga huyo.

 

Arsenal ilikuwa moja ya vilabu ambavyo vilikuwa vinawania saini ya aliyekuwa winga wa Leeds United ya nchini Uingereza Raphinha ambaye aliamua kutimkia katika klabu ya Barcelona ya nchini Uingereza.

Mikel Arteta anamtaka Pina kuongeza ubora katika kikosi chake

Mipango ya Kocha Mkuu wa klabu hiyo Mikel Arteta ni kuboresha eneo la ushambuliaji wa pembeni hivyo ameamua kuelekeza rada zake kwa winga huyo kutoka Villarreal.

 

Inasubiriwa kuona kama Villarreal watakubali ofa hiyo au watasimamia msimamo wa kutaka Arsenal ilipe kitita cha paundi milioni 80 kwa ajili ya kuvunja mkataba wake.

 

Tayari Arsenal imeshakamilisha dili la kuwasajili baadhi ya nyota akiwemo Gabriel Jesus kutoka klabu ya Manchester City.

Leave A Reply