Asahd: Mwaka Mmoja Anaogelea Umaarufu!

Asahd Khaled

USIKU wa Juni 23, 2016, akiwa ndani ya Studio za Televisheni ya Marekani ya ABC katika Kipindi cha Jimmy Kimmel Live, DJ ambaye pia ni rapa, DJ Khaled aliweka wazi kuwa mkewe, Nicole Tuck anatarajia kujifungua na angependa aoneshe ‘live’ kupitia Mtandao wa Snapchat tukio zima la kujifungua mtoto wake wa kwanza.

“The key is that I’m the king and every queen should support the king. I’m a talk to the doctor and if he says everything is going to run smooth, meaning that the queen is right and my son is right, if it’s running smooth … I can just do my thing.”(Lengo ni kwamba mimi ni mfalme na kila malkia lazima amuunge mkono mfalme. Mimi ndiye mwenye kuongea na daktari na akisema mke wangu yuko salama na mwanangu yuko salama na kwamba kila kitu kinakwenda salama, ninaweza kuendelea na mambo yangu.”)

Jumapili ya Oktoba 23, 2016 mchana DJ Khaled alitekeleza kile alichokuwa amekidhamiria na kupitia mtandao huo wa kijamii wa Snapchat watu wengi walikuwa wakifuatilia tukio moja tu la mkewe akijifungua.

Asahd Tuck Khaled ndilo jina alilopewa mtoto huyu na baba yake mara baada ya kuzaliwa ambapo Asahd ni neno la Kiarabu likimaanisha Simba lakini DJ Khaled amependelea kumuita Don na wakati mwingine Boss.

U-PRODYUZA

Kabla hajafikisha mwaka mmoja, tayari Asahd amekuwa supastaa ambapo DJ Khaled amempachika kama prodyuza wa albamu yake ya 10 iitwayo Grateful ikiwa na mastaa kibao kama vile Future, Travis Scott, Rick Ross, Migos, Chance the Rapper, Nicki Minaj, Kodak Black, Alicia Keys, Beyoncé, Jay-Z, Justin Bieber, Lil Wayne, 2 Chainz pamoja na Drake.

Licha ya kuwekwa kama prodyuza, katika albamu hiyo iliyoshika namba moja mara baada ya kutoka katika chati kubwa duniani za Billboard, picha ya Asahd imetumika katika kava na kumfanya kuhusika katika mauzo ya albamu.

HAKAMATIKI

Mara baada ya kuachiwa kwa Albamu ya Grateful, Asahd ametokelezea katika ubao mkubwa wa matangazo na wa gharama kuliko yote eneo la Times Square, New York, Marekani na picha yake kukaa kwa siku kadhaa.

ANA OFISI YAKE

Kama ulikuwa hujui, Asahd ni mmoja kati ya viongozi wakubwa katika Kampuni ya We The Best ya DJ Khaled na ndani yake ametengenezewa ofisi.

MASTAA WANAM-KUBALI

Asahd ni mtoto anayeongoza kwa kupendwa mitandaoni akiwa na wafuasi milioni 1.9 katika ukurasa wake wa Instagram. Mastaa kibao wameonesha hisia zao wazi za kumkubali kama vile Travis Scott, P Diddy, Justin Bieber, Rihanna, Marc Anthony, Kelvin Hart na wengine wengi.

ANA-MILIKI SAA YA MIL. 200

Katika kusherehekea kutimiza mwaka mmoja, shughuli yake iliendeshwa na P Diddy kama MC na siku hiyo DJ Khaled alimfanyia kufuru ya kumzawadia Asahd saa ya dhahabu aina ya Franck Muller yenye thamani ya dola za Kimarekani $100,000 (milioni 226 za Kibongo).

UBALOZI

Dogo amelamba shavu na kampuni kubwa ya mavazi duniani ya Gucci ambapo mara nyingi huonekan akiwa amevaa suti za Gucci zenye thamani ya dola za Kimarekani 2,500 hadi 4,000 (milioni 5 hadi 9 za Kibongo). Pia ni balozi wa brand ya kute

ngeneza viatu vya watoto vya Jordans pamoja na mavazi. Februari mwaka huu, katika maonesho ya mavazi yaliyofanyika Ukumbi wa Rookie, Marekani, alizindua viatu vyake vya watoto vijulika-navyo kama Jordan x Asahd vyenye thamani ya milioni mbili za Kibongo.

ALBAMU MPYA YUMO

Kuonesha kuwa DJ Khaled yupo siriazi na mafanikio ya Asahd, tayari ameshaingia chimbo na kutengeneza albamu mpya ya 11 iitwayo Father of Asahd ambapo dogo amewekwa pia kama prodyuza wa albamu hiyo.

Tayari ‘teaser’ ya ngoma mpya kutoka katika albamu hiyo iitwayo Top Off imeshaanza kuzagaa mitandaoni ambapo Asahd anaonekana katika video akijiachia juu ya ‘ndinga lake’.Top Off imewashirikisha Future, Beyonce na Jay Z.

ANDREW CARLOS


Loading...

Toa comment