The House of Favourite Newspapers

Asap Rocky Ajisogeza kwa Rihhana

0

MWANAMUZIKI wa miondoko ya Rnb Robyn Rihanna Fenty maarufu kama Rihanna na msanii wa Hip Hop Rakim Mayers A$AP Rocky wapo kwenye mahusiano ya kimapenzi, umethibitisha mtandao wa Page Six pamoja na mitandao mikubwa ya habari za burudani nchini Marekani.

 

Mitandao hiyo imeeleza kwamba imewanasa wawili hao wakila chakula cha usiku pamoja na marafiki mjini New York, hivi karibuni wiki iliyopita.

 

Kabla ya uthibitisho huu, Riri na Rocky walikuwa wakihisiwa muda mrefu kuwa kwenye mahusiano, hii ni tangu Rihanna aachane na bilionea Hassan Jameel mapema mwaka huu.  Ukaribu wao ulianza tangu mwaka 2013.

 

Hivi karibuni walishirikiana kwenye kampeni ya Fenty Skin line na walifanya mahojiano na Jarida la GQ na Vogue kwa ajili ya promosheni.

Leave A Reply