Asha Boko Afunguka Baada ya Kuolewa Mara ya Pili

 

MSANII wa filamu wa muda mrefu nchini, Asha Boko, siku ya leo Novemba 20, amefunga ndoa kwa mara ya pili na mume wake, Duwa Msafiri,  nyumbani kwao Mlandizi.

 

Amesema hakutaka ndoa yake ijulikane kwa sababu watu wangeweza kutia vizuizi isitokee na kesho watafanya sherehe ukumbini maeneo ya Bagamoyo.

 

“Ni kweli nimeolewa leo nyumbani kwetu Mlandizi, mume wangu anaitwa Duwa Msafiri na kesho kutakuwa na sherehe ukumbini maeneo ya Bagamoyo.  Nilikuwa sijatangaza kwa sababu nisingeolewa watu wangenitangaza ila taarifa nimetoa kwenye familia, ndugu, jamaa na marafiki, mume wangu siyo mtu maarufu hawawezi kumuiba kwa sababu hanajielewa,” amesema Asha.

 

Asha amefunga ndoa hiyo ikiwa ni mara yake ya pili baada ya mume wake wa kwanza kushambuliwa na majambazi hadi kufariki mwaka 2010 wakati walipovamiwa nyumbani kwao Kimara, Jijini Dar es Salaam.

Toa comment