The House of Favourite Newspapers

Msemaji wa Simba Azikwa Magomeni Dar (Picha +Video)

0
Msemaji wa Simba Sports Club, Haji Manara,  akitoa wasifu wa marehemu.

MAREHEMU Asha Muhaji (50) aliyekuwa ambaye mhariri wa magazeti ya michezo ya Kampuni ya Habari Cooparation, Dimba na Bingwa,  pia Afisa Habari wa  Simba Sports Club ya Dar es Salaam, leo Alhamisi amezikwa kwenye makaburi ya Mwinyimkuu, Magomeni,  Dar es Salaam.

Msiba ulifanyika nyumbani kwao Kijitonyama,  Dar s Salaam,  na kuhudhuriwa na wanahabari na wadau mbalimbali wa michezo ambapo makundi mbalimbali yalitoa salamu za rambirambi.

Mohammed Mharizo, mfanyakazi wa Kampuni ya Magazeti ya Habari Coopation, Bingwa, Dimba na Mtanzania akielezea jinsi walivyofanya kazi na Asha enzi za uhai wake.

Miongoni mwa waliohudhuria msiba huo ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Wallace Karia na Katibu wake, Wilfred Kidao, Msemaji wa Simba SC, Haji Manara, Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire,  wachezaji na wadau mbalimbali.

Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao,  akimzungumzia marehemu jinsi alivyoshirikiana na shirikisho hilo kufanikisha timu ya taifa na soka  nchini kwa  kufanya vizuri.

Akimuelezea marehemu enzi za uhai wake msibani hapo kwa niaba ya Kampuni ya Habari Cooparation, Mohammed Mharizo alisema yeye ni miongoni mwa watu wengi waliofundishwa kazi na marehemu ambaye hakuwa mchoyo wa kuwarithisha wengine kipaji chake.

Waombolezaji wakimkilia marehemu.
…Wakiuswalia mwili wa marehemu.
Mwili ukipelekwa kaburini.
Wafanyakazi wenzake wakilia kwa huzuni.
Rais wa TFF, Wallace Karia (kulia) na Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire,  wakiwa kwenye msafara kuelekea makaburini.

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS/GPL

Leave A Reply