The House of Favourite Newspapers

Ashushiwa kipigo kwa kumpiga mkewe

0

Jamaa mmoja mume wa mtu aliyetambulika kwa jina la Geofrey mkazi wa Geita amejikuta akishushiwa kipigo cha kufa mtu na majirani zake baada ya kumpiga mkewe nusu kufa bila sababu za msingi.

Akizungumza na paparazi wetu, mpashaji wetu kutoka eneo la tukio alisema kuwa awali Geofrey ambaye ni mlevi maarufu mtaani hapo, alikuwa na tabia ya kumshushia kipigo mkewe mara kwa mara kila anaporudi kutoka kilabuni bila kujali hali mbaya ya mkewe ambaye ana kichanga cha miezi miwili.

Mpashaji wetu anasema kuwa, siku ya tukio Geofrey kama kawaida yake alifika nyumbani kwake usiku wa manane akiwa ‘ameutwika’ na kumtaka mkewe amfungulie mlango. Baada ya kumfungulia kama kawaida yake alimvamia na kuanza kumshushia kipigo mfululizo hadi akazimia jambo lililowakera majirani zake ambao waliamua kumshushia kipigo cha mwizi Geofrey wakidai wameichoka tabia ya kumpiga mkewe hivyo wanampa onyo.

“Ndiyo tabia yake yaani unakuta anampiga mkewe usiku wa manane tena huku akimtukana, sasa juzi ndiyo akakutana na wanaume wenzake wakamnyoosha unaambiwa siku hizi mbili naona katulia heshima ipo kwa mkewe,” alisema mpashaji wetu.

Leave A Reply