The House of Favourite Newspapers

Polisi Afukuzwa Kazi kwa Kusababisha Kifo

0

POLISI  Zanzibar imemfuta kazi Askari wake Hussein Yahya Rashid (36) baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kusababisha kifo cha Mussa Suleiman mkazi wa Miembeni ambaye alituhumiwa kwa kosa la wizi.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Awadh Juma Haji, alithibitisha kufukuzwa kazi kwa askari huyo mwenye namba  3307412 tangu tarehe 6-11 mwaka jana.

 

hAJI alifafanua zaidi kwamba kosa la askari huyo ni kumkabidhi mtuhumiwa wa kosa la wizi kwa raia ambao walimshambulia hadi kusababisha kifo chake huko Ziwani Mjini Unguja.

 

Alisema askari huyo alitakiwa kumkabidhi mtuhumiwa mbele ya polisi au kituo chochote kile ili kupata hifadhi na kusubiri taratibu nyengine za upelelezi pamoja na kufunguliwa mashtaka.

 

Aliongeza kwamba siku zote wahalifu wanapotenda makosa kimbilio lao ni vituo vya ulinzi ikiwemo Polisi ambapo wanaamini kwamba hatua za kisheria zitafuatwa ikiwemo kufunguliwa mashtaka na si kuwapeleka mahali wakapigwe.

 

”Ni kweli Jeshi la Polisi limemfukuza kazi aliyekuwa askari wake Hussein Yahya Rashid ambaye alimkamata raia anayetuhumiwa na makosa ya wizi, sasa yeye badala ya kumpeleka katika kituo cha Polisi alimsalimisha kwa raia wenye hasira na kusababisha kifo chake, jambo ambalo ni hatari,” alisema Kamanda huyo.

 

Kamanda Haji alitoa wito kwa askari wengine wa Jeshi la Polisi kuzifahamu sheria zinazoliongoza jeshi hilo ambalo linafanya kazi zake kwa mashirikiano makubwa na raia katika mitaa na maeneo mbalimbali Unguja na Pemba.

 

Alisema majukumu ya polisi  ni kulinda usalama wa raia ambapo wananchi wanapobaini maisha yao yapo hatarini wanatakiwa kujisalimisha kwa taasisi hiyo kwa hatua nyingine zaidi za kisheria na si kuuawa.

 

”Jeshi la Polisi kazi yake kubwa ni kulinda usalama wa raia, maisha yao na mali zao,” alisisitiza Haji.

 

Hussein Yahya Rashid aliuwawa na wananchi wenye hasira baada ya kudaiwa alikwenda kuiba sehemu na hivyo polisi huyo alikwenda kumkamata na kuwakabidhi wananchi wenye hasira na kumpiga hadi kifo.

 

Leave A Reply