The House of Favourite Newspapers

Askari Polisi Ajiua kwa Risasi

ASKARI polisi wa kituo cha Polisi Natta,Wilayani Serengeti mkoani Mara, Nelson William,  amejiua kwa kujipiga risasi akiwa kazini jana Jumatano, saa 9 alasiri kwa madai ya ugomvi na mpenzi wake aitwaye Amina Adam Bakari.

 

Kabla ya kufanya uamuzi huo, Nelson anadaiwa alikuwa na ugomvi na mpenzi wake huyo,  hali iliyosababisha avunje vyombo vya ndani alivyomnunulia.  Jambo hilo lilisababisha dada huyo kumshataki mtuhumiwa (Nelson) ambaye aliagizwa kulipa fidia ya Sh. milioni 1.5.

 

Maelezo aliyoacha Nelson kwenye karatasi kabla ya kujiua yameeleza kuwa kitendo cha kulipishwa pesa kilimfanya achukie kwani vyombo alivinunua yeye na yeye ndiye alivivunja, hivyo alilazimika kukopa pesa hiyo ili kumlipa mpenzi wake.

 

Aidha, amesema kwa mwanamke huyo kuna baadhi ya vitu vyake vingine ambavyo ameomba vipelekwe Bariadi kwa kaka yake aitwaye Dickson huku akisisitiza ujumbe huo usomwe siku ya kuagwa kwake.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, RPC wa Mara Juma Ndaki amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema jeshi hilo linaendelea na uchunguzi zaidi.

 

 

Comments are closed.