The House of Favourite Newspapers

Askari JWTZ Afariki Akijiokoa Kubakwa na Fundi Ujenzi

ASKARI wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kambi ya Tabora, Esther Gway,  amefariki wakati akijiokoa katika tukio la ubakaji lililotekelezwa na kijana aliyedaiwa kuwa ni fundi ujenzi.

 

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Emmanuel Nley, tukio hilo lilitokea juzi Jumapili, Januari 27, 2019, saa moja usiku katika eneo la Kariakoo mjini humo na kwamba mtuhumiwa alimvizia mwanajeshi huyo akiwa nyumbani kwake muda huo na kumkaba shingo kisha kumuangusha chini na katika purukushani za kutaka kumbaka, huku akimkaba shingoni,  alisababisha kifo chake.

 

“Fundi huyo anayedaiwa alikuwa akijenga nyumba ya marehemu eneo la Kariakoo katika manispaa ya Tabora, tayari anashikiliwa na Jeshi la Polisi na tunaendelea na uchunguzi, ambapo tayari mwili wa marehemu upo katika uchunguzi pia hospitalini”, amesema Kamanda Nley.

 

Akizungumzia taratibu za maziko ya marehemu amesema kuwa baada ya uchunguzi, mwili wa marehemu utakabidhiwa kwa ndugu  na jeshi la polisi kwa taratibu za maziko.

LIVE: Rais MAGUFULI Akiwaapisha Majaji na Ma-DC aliowateua hivi karibuni

Comments are closed.