The House of Favourite Newspapers

Askari Waliotimiza Miaka 22 Kazini Watoa Msaada Kituo cha Watoto Yatima

0
Askari akitoa msaada kwa watoto yatima

ASKARI wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha waliotimiza miaka ishirini na mbili kazini wametoa msaada katika kituo cha Faraja Orphanage kilichopo shangalai Wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha ikiwa ni mchango wao kwa kituo hicho cha kulea watoto yatima na wahitaji.

 

Akiongea kwa niaba ya askari wenzake Sajenti MWANEMA amesema wameona ni vyema kutoa msaada huo ambao umenda sambamba na shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa kuwalinda kipindi cha miaka ishirini na mbili kazini.

 

Aidha amebainisha kuwa imekuwa ni utamadunia wa askari Polisi kutoa msaada kwa makundi yenye uhitaji ambapo amewaomba watu wengine kutoa walicho nacho kwa watoto wenye uhitaji katika vituo vya watoto yatima.

Askari wa jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha wametoa msaada katika kituo cha Faraja Orphanage

Nae Mkurungenzi wa faraja orphanage Mchungaji Faraja Malaki amewashukuru askari hao kwa mchango na msaada wao katika kituo hicho na kuwaomba wengine wenye moyo wa kujitoa wafike kituo cha faraja kusaidia watoto hao wenye uhitaji.

 

Nae Jephason Faraja ambae ameongea kwa niaba ya watoto wenzake wanaolelewa katika kituo hicho amewashukuru askari hao kwa kutoa msaada huo ambao umefanya wajisikie ni kundi linalokumbukwa katika Jamii.

Leave A Reply