The House of Favourite Newspapers

ASKOFU KAKOBE: “MAGUFULI Ole Wako, Mimi ni Mbishi Sana” – Video

ASKOFU Mkuu wa kanisa la Full Gospel Bible fellowship (FGBF), Zakary Kakobe, ameweka wazi kukoshwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli kwa kuweza kuingiza ndege nyingine ya Air Bus 220-300.
Askofu Kakobe ameyasema hayo leo katika mapokezi ya ndege ya sita zilizoingizwa nchini katika awamu ya uongozi wa Rais Magufuli huku akiliombea taifa kutoa maneno hayo.

“Mheshimiwa Rais mimi huwa ni mbishi kidogo na ukiniona nimekanyaga mahali kama hapa ujue umenikosha na sijui kama kuna watu wengine wamekoshwa kama Kakobe kwa ajili ya haya yanayotendeka.

 

“Na wengine wanasema mnamwabudu na kumsifu wakati hata Biblia inasema anayestahili heshima apewe heshima, hivyo unastahili zote. “Kwa nini tukusifie wakati tunalipa kodi…sifa sifa zote hizi za nini?”

Askofu Kakobe amesema suala la kuwakusanya watu wote bila kujali itikadi huo ndio uzalendo unaotakiwa.

 

“Ukiona hizi shangwe na vigelegele japo sio wote wanaokusifu ujue kuna watu wanashangilia kazi zako na leo tunakusihi ujipongeze, ulale na ujue wapo watu wanakushangilia kwa kazi zako,” amesema Kakobe.

 

ASKOFU KAKOBE – “MAGUFULI Ole Wako, Mimi ni Mbishi Sana”

 

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.