The House of Favourite Newspapers

Askofu kuliombea taifa mvua

0

1.Kutoka kushoto ni, Mwenyekiti wa Dood News For All Ministry, Charles Gadi, Mchungani James Manyama na Mchungaji Leonard Leonce Kajuna wa kanisa hilo.

Kutoka kushoto ni Askofu wa Good News For All Ministry, Charles Gadi, Mchungaji James Manyama na Mchungaji Leonard Leonce Kajuna wa kanisa hilo wakati wakielezea mipango yao ya kuliombea taifa.

2.Askofu Gadi (kushoto) akiendelea kutoa ufafanuzi wa jambo.

Askofu Gadi (kushoto) akitoa ufafanuzi wa jambo wakati akiongea na wanahabari leo.

3.Wanahabari wakichukua tukio.

Wanahabari wakichukua tukio hilo.

ASKOFU wa Kanisa la Good News For All Ministry, Charles Gadi kupitia huduma yake ya maombi maalum, amesema anaandaa maombi ya kumwomba Mungu alete mvua za kutosha katika msimu huu ili kuondokana na janga la ukame, njaa na upungufu wa nishati ya umeme.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Askofu Gadi amesema kuwa maombi hayo ya kuombea mvua yanatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Karimjee, Oktoba 21, mwaka huu kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 7 mchana ambapo viongozi mbalimbali wa kiserikali na madhehebu mbalimbali wanatarajia kushiriki.

Amesema wakati Rais Jakaya Mrisho Kikwete anaingia madarakani mwaka 2005/2006, Tanzania ilikumbwa na ukame uliosababisha njaa na mgao mkubwa wa umeme lakini kwa kushirikiana na viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali, walifanya maombi na hatimaye mvua zikaanza kunyesha.

Amesema kuwa maombi hayo yatasaidia kuleta mvua na kusaidia upatikanaji wa nishati ya umeme unaotokana na maji, wakulima na wafugaji na wanyamapori pia kuzidi kunufaika vya kutosha.

Aidha katika maombi hayo, Askofu Gadi amesema yataambatana na kuombea amani taifa letu hususan katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu ili uweze kuisha kwa amani na Mungu aweze kuwasaidia Watanzania kupata viongozi watakaosaidia kuendelea kusukuma gurudumu la maendeleo ya taifa letu kuanzia ngazi ya udiwani, ubunge hadi urais.

Askofu Gadi aliwasisitizia Watanzania kuwa kuna maisha baada ya uchaguzi hivyo wasitumie kipindi hiki kujenga uhasama usio na tija na kuvunja umoja wa kitaifa uliodumu kwa miaka mingi kwa sababu ya itikadi za vyama na wagombea wao.

NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply