The House of Favourite Newspapers

Askofu Mkuu Anglikana Ahitimisha Rasmi Utawala wa Askofu Mokiwa

KANISA la Anglikana leo limefanya Ibada kuu ya Kiaskofu ya kutwaa Dayosisi ya Dar es Salaam na kuhitimisha utawala wa aliyekuwa Askofu Mkuu,  Dk Valentino Mokiwa.

Ibada hiyo imeongozwa na Askofu Mkuu wa kanisa hilo nchini, Dk. Jacob Chimedelya katika Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano lililopo Posta jiji Dar.

Hata hivyo, Askofu Chimedelya amemteua Jerome Napeli kuwa Kaimu Kasisi Mkuu wa Dayosisi ya Dar es Salaam hadi pale kanisa litakapofanya uchaguzi wa kumpata mrithi wa Askofu Mokiwa.

GPL ilizungumza na baadhi ya waumini kuhusu uamuzi huo ambapo walimpongeza Askofu Chimedelya kwa kumaliza mgogoro huo.

“Askofu katenda haki, kwa mtu atakayeibuka na kuanzisha varangati tena basi, dola itadili naye,”alisema Joshua ambaye ni muumini.    

Picha/Habari: Gabrile Ng’osha-GPL

Comments are closed.