The House of Favourite Newspapers

Aslay Ataja Sababu za Kuwa Singo

0

MWANAMUZIKI Bongo Fleva, Aslay Isihaka ameeleza sababu ya kukaa bila mpenzi (kuwa singo), Aslay anasema kuwa, kwa sasa ameamua kuwa bize na mambo yake kwa sababu haoni faida ya kuwa na mwanamke maishani mwake.

Akistorisha na OVER ZE WEEKEND, Aslay ambaye aliachana na mpenzi wake wa muda mrefu aliyezaa naye mtoto mmoja wa kike aitwaye Moza, Kaitesy Abdul ‘Tessy Chocolate anasema kwa sasa anainjoi kinoma kwa sababu anaishi
maisha ambayo hayana stresi.

 

Kwa sasa ninainjoi sana kuishi maisha ya peke yangu, ninafanya kile ambacho ninakipenda, hakuna anayenipangia
maisha. Kwa sasa bado niponipo kwanza, sina haraka,” anasema Aslay anayefanya poa na Ngoma ya Unanikoleza

Stori: KHADIJA BAKARI

Leave A Reply