Kartra

Asukile Njia Panda

 

BAADA ya kufungiwa kucheza mechi tano na faini ya shilingi 500,000 kutoka kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kutoa lugha zisizofaa, beki wa Tanzania Prisons, Benjamini Asukile sasa atasubiri hatma yake kutoka TFF kama atacheza kwenye kikosi cha timu ya Taifa Soka la Ufukweni ‘beach soccer’.

 

Kocha wa timu ya taifa ya soka la ufukweni, Boniface Pawasa alisema uteuzi wa Asukile kwenye kikosi chake ulifanyika kabla ya kufungiwa na Kamati ya Mashindano ya TFF, hivyo wao pia wataangalia kama ataenguliwa kwenye kambi ya timu hiyo au atabaki.

 

“Tunasubiri mwongozo kutoka TFF kama tunaweza kumtumia au laa kwa sababu tulimwita kabla ya kuadhibiwa, kwahiyo wao ndiyo watatuambia kama amefungiwa na huku au kwenyye michezo tu ile mingine,” alisema Pawasa.

 

Asukile na wachezaji wengine walikuwa visiwani Zanzibar walikoweka kambi ya muda wakijiandaa na Fainali ya Mataifa ya Afrika ya Soka la Ufukweni (BAFCON) ambazo zinatarajiwa kufanyika Senegal mwezi ujao.


Toa comment