The House of Favourite Newspapers

Jide Ataja Sababu Wakongwe Wana Majina Magumu

USIONE vyaelea ujue vimeundwa! Mkongwe kunako Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Jide’ amefunguka kuwa, wanamuziki wa zamani (wakongwe) walijipa majina magumu kwa sababu walihaso mno kuufikisha muziki huu hapa ulipo.

 

Akipiga stori na Over Ze Weekend, Jide amesema, zamani ilikuwa mtu anahangaika kinoma ili kutoka kimuziki na kuhakikisha ngoma inatoboa na kukubalikana.

 

“Siku hizi husikii majina kama Komando, Afande, Inspector, Profesa, Mwanafalsafa na mengine magumumagumu kwa sababu ilikuwa ngumu kutoboa.

 

“Lakini siku hizi hawatumii nguvu kubwa ndiyo maana wana majina lainilaini maana tulishawawekea msingi,” amesema Jide au Jaydee au Binti Machozi au Komando au Anakonda.

STORI: IMELDA MTEMA

Comments are closed.