ATOLLSPEED HYBRID OVEN; MASHINE YA KUOKA MIKATE YENYE ‘MAAJABU’

HEBU vuta picha, unafanya biashara ya kuoka mikate, oda zimekuwa nyingi, wateja wanakusubiria, lakini uwezo wako wa kuzalisha ni mdogo, jasho linakutoka kutokana na joto kali ndani ya jiko lako la kuokea mikate, hujui cha kufanya! Inachanganya kichwa si ndiyo?

 

Basi kwa taarifa yako, Kampuni ya Uuzaji wa Vifaa vya Jikoni ya Uni Industries imekuletea jiko la kisasa la kuokea mikate (oven) lenye teknolojia ya hali ya juu, liitwalo Atollspeed Hybrid Oven, lenye uwezo wa kuzalisha mikate mara tatu zaidi ya oven za kawaida, ndani ya muda mfupi tu.

Jiko hili, ni la kidijitali kwani mfumo wake upo kama kompyuta, lina vitufe vya kubofya na ‘screen’ ndogo inayoonesha kiwango cha joto, kiwango cha mikate inayookwa, kiasi cha umeme unaotumika na kadhalika.

“Ni mashine nzuri sana kwa wajasiriamali wadogo na wakubwa, wamiliki wa hoteli na wafanyabiashara wa bidhaa za kuokwa, inaweza kutumika hata maeneo ya vijijini kwa sababu inatumia umeme mdogo wa Volti 230 na inaweza kumpa mfanyabiashara faida kubwa kwa sababu inazalisha mikate kwa wingi kwa kutumia umeme kidogo na muda mfupi,” alisema Roscoe Bremer, Meneja wa Kanda wa Uni Industries.

 

Kwa mahitaji ya vifaa vingine vingi vya kisasa, tembelea maduka ya Uni Industries yaliyopo Staywell Complex, plot 1720, Haile Sellasie Road, mkabala na Marrybrown, Namanga jijini Dar es Salaam na Forodhani, Zanzibar.

 

Bidhaa nyingine zinazopatikana Uni Industries ni pamoja na vifaa mbalimbali kwa matumizi ya jikoni kama vile mashine za kisasa za kuoka vyakula, kupikia keki, kukata mbogamboga na matunda, kutengenezea juisi na kadhalika.

Lakini pia wanauza vifaa vingine kama majokofu ya kisasa ya ukubwa tofautitofauti, vifaa vya kusambazia vyakula kwenye sherehe na shughuli mbalimbali (catering services), mashine za kufulia, vifaa vya supermarket kama ‘shelves’ za kisasa, vitoroli vya kubebea bidhaa supermarket, samani za ndani na vingine vingi.

Pia unaweza kuwasiliana nao kwa simu namba 0681 111 999 au 0766 075 031

au kwa barua pepe adil@uni-tanzania.com.

Pia unaweza kutembea website yao kwa kubofya www.uni-eastafrica. com. Wahi sasa ili uwe miongoni mwa watu wanaokwenda na wakati kwa kumiliki vifaa vya kisasa vyenye teknolojia ya hali ya juu.

 

VIDEO: TAZAMA VIDEO YA VIFAA VYOTE KUTOKA UNI INDUSTRIES


Loading...

Toa comment