Auawa kwa Kupigwa Risasi Kagera

MTU mmoja amefariki dunia baada ya kupigwa risasi katika vurugu zilizotokea kati ya wakulima na walinzi wa wawekezaji wa mifugo katika eneo la Rutoro mkoani Kagera.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Awadhi Juma Haji amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kwamba chanzo cha vurugu hizo, ni wakulima kuvamia kitalu cha mfugaji katika eneo la Rutoro wakiwa na silaha za jadi na kuanza kushambuliana na walinzi.

 

Ameongeza kuwa katika mashambuliano hayo, walinzi hao waliokuwa na bunduki, walifyatua risasi iliyosababisha kifo cha mfugaji huyo na kwamba uchunguzi zaidi kuhusu tukio hilo unaendelea.


Toa comment