The House of Favourite Newspapers

Aucho Aupiga Mwingi Uganda, Yanga Wapagawa

0

PAMOJA viongozi wengi wa Yanga, kutojua zaidi uwezo wa kiungo wao mpya raia wa Uganda, Khalid Aucho, mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji, Dkt. Athumani Kihamia, ameonyesha wazi kuchanganyikiwa juu ya usajili wa kiungo wao mpya.

 

Alhamisi iliyopita Aucho alionyesha uwezo mkubwa wakati ailipokuwa akiichezea timu yake ya taifa ya Uganda dhidi ya Timu ya taifa ya Kenya ‘Harambe Stars’, jambo lililowainua mashabiki wengi na kuwa na imani naye tangu aliposajiliwa.

 

Hivi karibuni usajili wa Aucho ulizua gumzo kubwa baada ya taarifa kueleza kwamba ITC yake ilicheleweshwa, huku wengine wakifikia hatua ya kudai kuwa endapo kibali hicho hakikufika kwa wakati basi nyota huyo hatapata muda wakuichezea Yanga mechi za awali za Michuano ya Kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Dkt Kihamia, alisema kuwa wale waliokuwa hawajamuona nyota huyo basi wanatakiwa wavimbe kwani ni moja ya usajili bora.

 

“Hakika sasa ninaimani kubwa na usajili wetu wa Aucho maana nimemuona ni hatari kiasi kwamba hata Wanayanga wenzetu ambao hawajamuona wanatakiwa wavimbe kwani usajili pekee wa Yanga bora sana kutokea ni huo, ndio maana kamuweka benchi Lwanga, (Tadeo wa Simba), hivyo Mwanayanga hatakiwi kutembea kinyonge baada ya usajili wa nguvu kama huu,”alisema.

MUSA MATEJA, Dar es Salaam

 

Leave A Reply