The House of Favourite Newspapers

Aucho, Bangala Waiwahi Azam FC

0

UONGOZI wa Yanga, umeweka wazi kuwa wachezaji wao Khalid Aucho, Yanick Bangala, Djuma Shabani
na Mukoko Tonombe,
watapatikana katika mchezo unaofuata wa nusu fainali ya Kombe la mapinduzi dhidi ya
Azam FC.


Yanga imetinga hatua hiyo
mara baada ya kumaliza vinara wa Kundi B kwa kukusanya pointi nne na kesho Jumatatu
itacheza dhidi ya Azam FC.


Akizungumza na Spoti
Xtra, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, aliweka wazi kuwa: “Wachezaji wetu ambao
walijiunga na timu ya taifa ya
DR Congo, Yanick Bangala, Djuma Shabani na Mukoko Tonombe tayari wameshamaliza mechi yao ya timu ya taifa Januari 6, hivyo itawachukua siku mbili mpaka kufika huku Zanzibar.


“Aucho pia atapatikana katika
mchezo unaofuata mara baada ya kumalizika kwa mapumziko yake nchini Uganda, hivyo wapenzi wa Yanga wasiwe na wasiwasi kwani malengo yetu ni yale yale kuhakikisha kuwa tunatwaa ubingwa huu.”

“Tumefanya mabadiliko kidogo ya kikosi kwa ajili ya kuwalinda wachezaji wetu na majeraha na kuwapa naafasi wengine wacheze ila haina maana hatutaki ubingwa. Wanasimba wawe na imani kuwa tutafanya
vizuri.”


Kesho Jumatatu, Simba
wanatarajiwa kucheza nusu fainali dhidi ya Namungo, kama watashinda watacheza
fainali na mshindi kati ya
Yanga na Azam FC.

 

Leave A Reply