The House of Favourite Newspapers

Aucho, Bangala Wakomaliwa Yanga

0
KOCHA Mkuu wa Yanga, Mtunisia, Nasreddine Nabi, ni kama ameshtukia kitu baada ya kuwafanyisha wachezaji wake mazoezi ya fitinesi kila siku asubuhi, huko Avic Town, Kigamboni, Dar.
 
Hiyo ikiwa ni siku chache tangu kocha huyo atupiwe lawama wachezaji wake kukosa fitinesi huku kipindi cha pili katika mechi kuishiwa pumzi.
Kati ya wachezaji wanaokomaliwa na kocha huyo ni viungo wake, Khalid Aucho, Yannick Bangala na Feisal Salum ‘Fei Toto’.
 
Akizungumza kwa niaba ya kocha huyo, Kocha Msaidizi wa Yanga, Mrundi, Cedric Kaze, alisema timu yao hivi sasa imeingiza program ya gym kila siku kwa lengo ya kutengeneza fitinesi.Kaze alisema program hiyo waliianza wiki iliyopita am-bayo wameen-delea nayo wiki hii kwa kuanzia jana Jumatatu.
Aliongeza kuwa, jana walifanya mazoezi ya gym asu-buhi kabla ya jioni kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya JKT Tanzania.
 
“Gym imeingia katika program ya mazoezi yetu ya kila siku asubuhi kwa kufanya mazoezi ya nguvu kwa ajili ya kuongeza fitinesi, tunataka kuona wachezaji wakicheza kwa spidi tukiwa na mpira.“
 
Tumepata taarifa za wachezaji wetu kuchoka katika kipindi cha pili, kama benchi tumeliona hilo na tunalifanyia kazi ili kuhakikisha wachezaji wetu wanaimarika,” alisema Kaze.
STORI: WILBERT MOLANDI, Dar


Leave A Reply