The House of Favourite Newspapers

Aucho Jeuri Nyie! Atupa Kijembe Simba

0

BAADA ya kumaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara bila ya kufungwa huku wakiwa kileleni katika msimamo wakiwa na pointi 39, kiungo fundi wa Yanga, Mganda, Khalid Aucho ameibuka na kutamka ligi wataianza rasmi Februari 27, mwaka huu.

 

Yanga tarehe hiyo ambayo ni keshokutwa Jumapili wanatarajiwa kucheza mchezo wa kwanza wa raundi ya pili ya ligi dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, na kauli hiyo ya Aucho ni kama anawaambia Simba wasahau suala la ubingwa msimu huu kwani kazi ndio kwanza inaanza.

 

Kauli ya Mganda huyo imekuja baada ya kufanikiwa kuwafunga Mtibwa Sugar mabao 0 2-0 nyumbani kwao kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.

Ushindi huo umewawezesha timu hiyo kuwaacha watani wao, Simba kwa tofauti ya oint inane. Kwa mujibu wa Aucho, baada ya mchezo dhidi ya Mtibwa nguvu na akili zao wanazielekeza katika mchezo ujao wa ligi dhidi ya Kagera ambao ni muhimu kwao kupata matokeo mazuri.

 

Aucho alisema kuwa katika kuelekea mchezo huo wataingia uwanjani kusaka pointi tatu kama vile ndiyo wanaanza ligi.

 

. “Wachezaji wote tumesahau matokeo tuliyoyapata katika mzunguko wa kwanza wa ligi, badala yake tutaingia kutafuta pointi tatu Februari 27.

 

“Hivyo mchezo wetu ujao wa ligi (Kagera) tutaingia uwanjani kwa lengo moja pekee kupata ushindi. Na tutauchukulia mchezo huo kama vile tunaanza ligi.

 

“Nafikiri nitakuwa nimeeleweka vizuri nina maana gani, kama inavyojulikana malengo yetu katika msimu huu ambao kwetu tunahitaji kuchukua makombe yote, nimalizie kwa kuwaambia nawapenda mashabiki wa Yanga” alisema Aucho.

STORI: WILBERT MOLANDI, CHAMPIONI IJUMAA

ASEE! HII VIVO 23 ni ZAIDI YA SIMU, ‘CAMERA’ YAKE NI YA KIBABE, ZAWADI KIBAO KWA WATEJA WA KWANZA..

 

Leave A Reply