The House of Favourite Newspapers

Aucho Rasmi Aripoti Kambini Morocco

0

KIUNGO mkabaji wa Yanga, Mganda Khalid Aucho juzi aliripoti kambini nchini Morocco sambamba na kuanza mazoezi ya pamoja na wenzake.

 

Hiyo ni ikiwa siku chache tangu timu hiyo imepiga kambini nchini huko wiki iliyopita. Ujio wa Aucho kumenogesha kambi ya timu hiyo ambaye yeye pekee ndiye alikuwa hayupo baada ya juzi beki Mkongomani, Yannick Litombo kuripoti.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Meneja Mkuu wa timu hiyo, Hafidh Saleh alisema kuwa kiungo huyo tayari ametua kambini. Saleh alisema kuwa kiungo huyo jana Jumapili alianza mazoezi ya pamoja na wenzake.

 

“Aucho yupo kambini tangu juzi (Jumamosi) na leo (jana), alianza mazoezi mepesi ya binafsi asubuhi. “Jioni anatarajiwa kufanya kwa mara ya pili na wenzake katika kujiweka fiti ili aendane na wenzake baada ya kuchelewa kuripoti kambini,” alisema Saleh.

WILBERT MOLANDI na Ibrahim Musa

Leave A Reply