AUNT ACHARUKA KUAMBIWA YUKO NA KIBENTENI

 MSANII wa filamu Bongo Muvi, Aunt Ezekiel amewacharukia watu wanaosema kuwa anapenda kutembea na ‘vibenteni’ kama ilivyo kwa mwanaume wake mpya na kuwaambia kuwa hayo ni maisha yake na hata kama ni mdogo hajamzaa yeye hivyo watu waache kumpigia kelele.

 

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Aunt alisema kuwa watu wengi wanapenda kuzungumza vitu lakini hakuna hata mmoja anayejua vitu hivyo kwa undani na hata huyo mpenzi wake mpya wanaomsema ni kibenteni hawajui umri wake.

 

“Utasikia mtu oooh kibenteni, kwani nimemzaa mimi jamani au kuna mtu ana kadi yake ya kliniki ambayo inasema umri wake yaani watu wakizoea maneno hawaachi hata kidogo kusema na mimi nawaacha waropoke tu,” alisema Aunt ambaye alikuwa ni mzazi mwenzie na dansa mahiri wa Kruu la Wasafi Classic Baby (WCB), Moses Iyobo.


Loading...

Toa comment