AUNT AFUNGUKA ISHU YA MUMEWE KUTOKA JELA

 STAA wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel amedai kuwa madai ya mumewe Sunday Demonte kutoka gerezani nchini Dubai alikokuwa amefungwa anayasikia tu kwa watu lakini anachoamini yeye ni uzushi.  Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Aunt alisema: “Asingeweza kutoka bila mimi kujua kwa hiyo hizo  habari ni uzushi mtupu, mimi nazisikia tu na wala sijui zinatoka wapi,” alisema Aunt.

Madai ya kutoka jela kwa Sunday yaliibuka wiki iliyopita huku ikielezwa kuwa, muda wake wa kifungo ulikuwa umeisha na hata alipotoka, alifichwa kwanza. Gazeti hili linaendelea kufanyia kazi madai hayo na kitakachobainika kitawekwa bayana.


Loading...

Toa comment