The House of Favourite Newspapers

Aunt amfundisha ulevi Moze

aunty33Staawa Bongo Movie, Aunt Ezekiel akiwa na mpenzi wake Moses Iyobo ‘Moze’.

STAA wa Bongo Movie, Aunt Ezekiel juzi kati baada ya kujitwika kilaji a.k.a masanga vilivyo, alijikuta akijigamba waziwazi kumfundisha ulevi mzazi mwenzake, Moses Iyobo ‘Moze’.

Akichonga na kona ya Bongo Movie kwa sauti ya kilevi, Aunt alikiri kuwa mnywaji mzuri wa pombe hivyo kwenye maisha yake hategemei kukaa na mume zaidi ya miaka miwili halafu ashindwe kumshawishi kunywa naye pombe kwani huo utakuwa ni uzembe wa hali ya juu.

“Nimejitahidi sana kumuwezesha Moze wangu kuanza alau kugusa kinywaji kilaini maana zamani kila nikimpatia pombe lazima akasirike. Nafurahi kuona sasa ameanza kuonjaonja hadi inafikia hatua anamaliza hadi chupa tatu,” alisema Aunt.

Kwa upande wa Mose Iyobo alisema kwa sasa anakunywa bia tatu tu!

Comments are closed.