The House of Favourite Newspapers

Aunt atuhumiwa ushirikina

0

auntMoses Iyobo na Aunt Ezekie.

Imelda Mtema

MAKUBWA! Mzazi mwenziye na dansa wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Moses Iyobo, Mwengi amemtuhumu mwigizaji Aunt Ezekiel kuwa ni mshirikina akidai amemrogea mwanaye.

iyoboMoses Iyobo na Mwengi samabamba na mtoto wao.

Mwengi alisema hivi karibuni alimpeleka mwanaye nyumbani kwa Aunt ili akamuone baba yake (Iyobo), lakini alipomrudisha alikuwa katika hali mbaya.

“Mtoto karudi anaumwa, tumeenda hospitali hatukuona tatizo hadi kwa wataalam wa jadi ndiko tulikopata suluhu, ni Aunt tu atakuwa kamfanyia figisufigisu,” alisema Mwengi.

Baada ya Mwengi kumwaga madai hayo kwa Risasi Jumamosi, mwanahabari wetu alimpigia simu Aunt ambapo alipopatikana, alimpuuza mwanamke huyo kwa kujibu kwa kifupi.

“Huyo anatafuta kiki kupitia jina langu, nimroge yeye kwa lipi? Si bora niwaroge watu wazima kuliko yeye mwendawazimu.”

Leave A Reply