The House of Favourite Newspapers

Aunt, Bwana’ke Mpya Wanaswa Live Airport, Aonyesha Dole la Kati – Video

BAADA ya stori nyingi kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Staa wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel ameachana na mpenzi wake, Mose Iyobo na sasa anabanjuka na mshikaji mwingine ambaye picha zao zimetrendi kwenye mitandao wikiendi iliyopita, Global TV Online imemnasa msanii huyo akiwa na bwana’ke huyo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

 

Aunt na bwana’ke wamenaswa leo Jumatatu, Aprili 22, 2019  wakati akimsindikiza jamaa huyo aliyekuwa akisafiri kutoka nje ya jiji la Dar es Salaam.

 

Baada ya Global TV Online kuomba kuzungumza naye ili awaeleze mashabiki zake ukweli kuhusu yanayoendelea mitandaoni, msanii huyo alikataa kuzungumza huku akinyoosha kidole cha kati jambo ambalo tafsiri yake ni kutukana.

 

TAZAMA VIDEO HII

Comments are closed.