The House of Favourite Newspapers

Aunt, Iyobo Wafanya Tambiko Mapangoni

0

TANGA: MUIGIZAJI Aunt Ezekiel na mzazi mwenziye Moses Iyobo wamefanya ziara kwenye mapango ya Amboni jijini Tanga ambapo pamoja na mambo mengine, wamefanya tambiko ili penzi lao lisiingie tena ‘kidudu mtu’ likavunjika tena.  Baada ya wawili hao kutinga kwenye mapango hayo, walipata maelekezo na kuambiwa kuwa kama wana imani na mizimu chochote wakikiomba watafanikiwa hivyo walijiongeza na kuzama ndani kwenda kutambikia penzi lao lisitetereke tena.

Baada ya kupata maelekezo hayo, waliongozana kwenda ndani pamoja na watoto wao na kupanda mpaka juu kwenye pango ambalo lina taswira ya Bikira Maria na kuanza kuomba ili kidudu mtu asiingie tena kwenye penzi lao. Baada ya kutoka ndani ya mapango hayo, wote kwa pamoja walionekana wenye nyuso za furaha wakafunguka mbele ya Risasi Mchanganyiko kwamba wameanza maisha mapya.

“Nimefurahi na watoto wangu wamefurahi pia, lakini tumeomba amani kwenye mapenzi yetu ili tusigombane tena au kuachana kama ilivyowahi kutokea mwaka jana,” alisema Aunt. Kwa upande wake Iyobo alisema ana imani kwa jinsi walivyoelezwa kuwa maombi yao yatapokelewa na (mizimu) pia kuinjoi pamoja na familia.

“Kwa kweli nimefurahi sana naamini tulichoomba kimepokelewa kwa sababu napenda familia yangu,” alisema Iyobo. Takriban miezi sita iliyopita wawili hao walikuwa kwenye mgogoro mkubwa mpaka kufikia hatua ya kutengana na kila mmoja kushika hamsini zake, hata hivyo walirudiana na sasa mapenzi ni motomoto.

Stori: IMELDA MTEMA, RISASI

Leave A Reply