AUNT: JAMANI MWACHENI MWANANGU

Aunt Ezekiel

CHONDECHONDE! Staa wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel amewaomba baadhi ya watu kuacha kumsimanga mwanaye, Cookie kuhusiana na nywele zake kwa sababu yeye ndiye ana uchungu na siyo mtu mwingine. Akizungumza na Gazeti la Ijumaa, Aunt alisema kuwa hakuna kinachomkera kama mtu kumzungumzia mtoto wake au kumfundisha jinsi ya kumuweka wakati wengine watoto wao wanashindwa kuwaweka kama wao wanavyotaka.

“Jamani nikiweka nywele yoyote kichwani kwa mwanangu, nikimbana shida, jamani naomba ieleweke ni mwanangu hivyo waniachie hata nikimfunga katani ni uamuzi wangu,” alisema Aunt aliyemzaa mtoto huyo na dansa wa WCB, Moses Iyobo.


Loading...

Toa comment